.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Sports(Michezo). Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Sports(Michezo). Onyesha machapisho yote

Alhamisi, 5 Januari 2017

Chapecoense kusajili wachezaji 20 wapya

Januari 05, 2017 0
Chapecoense kusajili wachezaji 20 wapya
Uongozi wa klabu ya soka ya Chapecoense ya Brazil ambayo ilipoteza wachezaji wake 19 kwenye ajali ya ndege iliyotokea mwezi Novemba mwaka jana, umepanga kusajili wachezaji wengine 20 kwa ajili ya kuziba nafasi hizo.
Wachezaji wawili walionusurika katika ajali hiyo kati ya watatu akiwemo Neto na Alan Ruschel wanatarajiwa kuwa miongoni mwa wachezaji watakaoichezea timu hiyo, kwa mujibu wa Mkurugenzi wa timu hiyo Rui Costa.
“More than a tribute, we expect Alan and Neto to come back and wear them. Follmann sadly won’t be able to but he will certainly be back here with us in some capacity. The only ones that can wear those jerseys are them,” amesema Costa.
Timu hiyo inatarajiwa kucheza mechi yao ya kwanza kwa msimu huu Januari 26 wakiwa nyumbani dhidi ya Joinville.

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Google Play Store na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka HabNews Tv    

Alhamisi, 3 Novemba 2016

David Moyes nje mechi moja FA

Novemba 03, 2016 0
David Moyes nje mechi moja FA
Kocha wa Sunderland David Moyes amepigwa marufuku mechi moja na chama cha soka cha England kwa kutumia lugha ya matusi dhidi ya mwamuzi wa mechi amepigwa na faini ya £8,000.
39d7652100000578-3897342-image-a-53_1478089106440
Kisa hicho kilitokea baada ya refa kunyima Sunderland mkwaju wa penalti dakika ya 90 mechi ya Jumatano wiki iliyopita ambapo klabu hiyo ilifungwa 1-0 na Southamptn Kombe la FA.
Baada ya mechi hiyo, Moyes alisema: “Tatizo lilitokea aliponiandama hadi pahala nilipokuwa nimesimama. Nilitumia lugha ya matusi na sikufaa kufanya hivyo.”
Moyes tokea ameteuliwa kuwa meneja wa Sunderland Julai na ameshinda alama mbili pekee kutoka katika mechi 10 za ligi.

Bonyeza HAPA kudownload application yetu na upate habari punde zitufikiapo

Jumamosi, 22 Oktoba 2016

Wachezaji wa Manchester United waoneshana ubabe wa magari mazoezini

Oktoba 22, 2016 0

Hapa Kazi tu!, José Mourinho na kikosi chake cha Man united kimeonyesha hakuna kumpumzika zaidi ya kupiga mazoezi mwanzo mwisho kwa ajili ya kujiandaa kuivaa klabu ya Chelsea siku ya jumapili.
Sasa katika kuelekea kiwanja cha Mazoezi, kila mchezaji wa Man United alionesha mbwembwe za kuja na ndinga ya Kifahari, Sasa hebu niambie nani ametisha hapa.
Anthony Martial arrived at training in a Smart Car on Thursday
Anthony Martial aliingia na ndinga ya Smart Car
Morgan Schneiderlin has mustered just five minutes of league action
Hilo ndinga la Morgan Schneiderlin likiwa linawasili hapo
Eric Bailly arrived to training being chauffeured by his dad
Eric Bailly yeye hakuwa na mbwembwe sana, alishushwa na Range Rover akiwa na Baba yake ambaye alikuwa anaendesha ndinga hiyo.
Sergio Romero shares the same taste with his team-mate in supercars
Sergio Romero nae akaingia na ndinga yake ya Lamborghini

Henrikh Mkhitaryan arrives in his £260,000 Lamborghini
Hii ni ndinga ya Henrikh Mkhitaryan aliyoingia nayo kwenye mazoezi, gari hili ni moja ya magari ambayo yenye thamani kubwa “Lamborghini”

Jumanne, 6 Septemba 2016

TOP 10 ya wanasoka wanaolipwa mkwanja mrefu

Septemba 06, 2016 0
TOP 10 ya wanasoka wanaolipwa mkwanja mrefu
james-rodriguez-top-model_adpo15cd890c1rrua6un2uy88-768x461


Leo September 6 2016 nimekutana na list ya TOP 10 ya mastaa wa soka wanaongoza kwa kulipwa mkwanja mrefu, list kutoka mtandao wa www.alux.com hadi kufikia August 2016 hii ndio ilikuwa list ya wanasoka wanaoongoza kwa kulipwa mkwanja mrefu.

10. James Rodriguez ($21 million zaidi ya Tsh bilioni 45)

james-rodriguez-top-model_adpo15cd890c1rrua6un2uy88-768x461
James Rodriguez

9. Cesc Fabregas ($21 million bilioni zaidi ya Tsh bilioni 45)

Cesc-x-Beats-Hear-What-You-Want-1-768x575
Cesc Fabregas

8. Eden Hazard ($22 million zaidi ya Tsh bilioni 48)

hazard1-768x435
Eden Hazard

7. Luis Suarez ($23 million zaidi ya Tsh bilioni 50)

13934991186929-768x511
Luis Suarez

6. Sergio Aguero ($24 million zaidi ya Tsh bilioni 52)

pepsiAGUERO-DC-PORTRAIT_LR-768x765
Sergio Aguero

5. Wayne Rooney ($26 million zaidi ya Tsh bilioni 56)

wayne_rooney_fc247_1_18948-768x480
Wayne Rooney

4. Gareth Bale ($34 million zaidi ya Tsh bilioni 74)

Gareth-Bale-on-holiday-in-Marbella-768x534
Gareth Bale

3. Neymar Jr. ($36 million zaidi ya Tsh bilioni 78)

Neymar-Jr-8450_klein-768x512
Neymar Jr.

2. Lionel Messi ($77 million zaidi ya Tsh bilioni 168)

tumblr_mcauq5tifs1r38yfko1_1280-768x489
Lionel Messi

1. Cristiano Ronaldo ($82 million zaidi ya Tsh bilioni 179)

wx-768x497 (1)
Cristiano Ronaldo

Ijumaa, 26 Agosti 2016

Ronaldo atwaa tuzo ya mchezaji bora Ulaya

Agosti 26, 2016 0

Nahodha wa timu ya taifa ya Ureno anayeichezea klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo usiku wa August 25 aliingia katika historia mpya ya soka lake, hiyo inatokana na kushinda tuzo ya mchezaji bora wa ulaya wa mwaka kwa kuwashinda wapinzani wake Antoine Griezmann wa Atletico Madridi na timu ya taifa ya Ufaransa, pamoja na Gareth Bale.
3794A4FB00000578-3758562-image-a-9_1472143267089
Kutoka kushoto ni Bale, Ronaldo na Griezmann
Ronaldo anafanikiwa kushinda tuzo hiyo baada ya kumaliza msimu wa 2015/2016 kwa mafanikio makubwa ikiwemo kuiwezesha Real Madrid kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa barani Ulaya na kufikisha rekodi ya kutwaa Kombe hilo mara tatu katika historia yake ya soka.
3795021500000578-3758562-image-a-16_1472147165310
Hata hivyo msimu wa 2015/2016 licha ya kuiwezesha Ureno kutwaa taji la Euro 2016 kwa mara ya kwanza katika historia, Ronaldo akiwa na Real Madrid msimu wa 2015/2016 alikuwa kafunga jumla ya goli 51 katika mechi zake 48 alizocheza pamoja na kutoa assist 15, lakini akiwa na rekodi ya kufunga magoli 16 katika mechi 12 za UEFA Champions league.

3794A15300000578-3758562-image-a-5_1472141905887

37949DC600000578-3758562-Ronaldo_signs_autographs_for_fans_before-a-7_1472142976665
37948A0600000578-3758562-image-a-10_1472143292511

Jumanne, 23 Agosti 2016

Hivi ndivyo baadhi ya mataifa ya Afrika yalivyoorodheshwa katika jedwali la medali katika michezo ya Rio de Janeiro iliokamilika.

Agosti 23, 2016 0
Baadhi ya mataifa ya Afrika yalivyoorodheshwa katika jedwali la medali katika michezo ya Rio iliokamilika.
KENYA ilikuwa katika nafasi ya 15
DHAHABU:
Jemima Sumgong - Marathon ya wanawake
David Rudisha - Mita 800 wanaume
Faith Kipyegon - Mita 1500 wanawake
Conseslus Kipruto -Mita 3000 wanaume kuruka viunzi na maji
Vivian Cheruiyot - Mita 5000 wanawake
Eliud Kipchoge - Marathon wanaume
FEDHA:
Paul Tanui - Mita 10,000 wanaume
Vivian Cheruiyot - Mita 10,000 wanawake
Hyvin Kiyeng - Mita 3,000m kuruka viunzi na maji-wanawake
Boniface Mucheru Tumuti - Mita 400m kuruka viunzi-wanaume
Hellen Obiri - Mita 5000-wanawake
Julius Yego - Kurusha mkuki-wanaume
SHABA:
Margaret Wambui - Mita 800-wanawake
(Alipokonywa medali -Ezekiel Kemboi - Mita 3000 kuruka viunzi na maji
AFRIKA KUSINI ilikuwa katika nafasi ya 30
DHAHBU:
Wayde van Niekirk - Alivunja rekodi ya dunia-Mita 400-wanaume
Caster Semenya - Mita 800-wanawake
FEDHA:
Cameron Van Der Burgh - Mita 100 Breaststroke-wanaume
Chad Le Clos - Mita 200m Freestyle-wanaume
Lawrence Brittain & Shaun Keeling - Kupiga makasia-wanaume
Chad Le Clos - Mita 100 Fly- wanaume
Luvo Manyonga - Long Jump- wanaume
Sunette Viljoen - Kurusha mkuki-wanaume
SHABA:
Rugby Sevens - Wanaume
Henri Schoeman - Triathlon -Wanaume
ETHIOPIA ilikuwa katika nafasi ya 44
DHAHABU:
Almaz Ayana - Mita 10,000 wanawake - Rekodi ya dunia
FEDHA:
Genzebe Dibaba - Mita 1500- wanawake
Feyisa Lilesa - Marathon -wanaume
SHABA:
Mare Dibaba - Marathon- wanaume
Tamirat Tola - Mita 10,000 -wanawake
Tirunesh Dibaba - Mita 10,000- wanawake
Almaz Ayana - Mita 5000- wanawake
Hagos Gebrhiwet - Mita 5000- wanaume
IVORY COAST ilikuwa katika nafasi ya 51.
DHAHABU:
Cheick Sallah Cisse - Taekwondo-Wanaume chini ya kilo 80
SHABA:
Ruth Gbagbi - Taekwondo- Wanawake chini ya kilo 67
ALGERIA equal 62nd on overall Medal table:
FEDHA:
Taoufik Makhloufi - Mita 800- wanaume
Taoufik Makhloufi - Mita 1500- wanaume
BURUNDI ilikuwa ya 69
FEDHA:
Francine Niyonsaba - Mita 800-wanawake
NIGER ilikuwa katika nafasi ya 69
FEDHA:
Abdoulrazak Issoufou Alfaga-Taekwondo-wanaume chini ya kilo 80
MISRI ilikuwa katika nafasi ya 75
SHABA:
Sara Ahmed - Kubeba uzani kilo 69
Mohammed Mahmoud - Kubeba uzani kilo 77
Hedaya Wehaba -Taekwondo wanawake kilo 57
TUNISIA ilikuwa katika nafasi ya 75
SHABA:
Ines Boubakri - Fencing- Wanawake
Marwa Amri - Miereka -Wanawake kilo 58
Oussama Oueslati - Taekwondo -wanaume chini ya kilo 80
MOROCCO ilikuwa nafasi ya 78
SHABA:
Mohamed Rabii - Masumbwi uzani wa Welterweight
NIGERIA ilikuwa katika nafasi ya 78
SHABA
Timu ya kandada ya -wanaume

Jumapili, 21 Agosti 2016

Neymar ameiongoza Brazil kushinda medali ya dhahabu Olympic katika soka

Agosti 21, 2016 0

Wakati Ligi Kuu mbambali dunia zikiendelea August 20 2016, katika uwanja wa Maracana Rio de Janeiro Brazil timu ya taifa ya nchi hiyo inayoshiriki Olympic ilicheza mchezo wa fainali ya Olympic dhidi ya timu ya taifa yaUjerumani, huu ulikuwa ni mchezo ambao ulihudhuriwa na mwanariadha wa JamaicaUsain Bolt.
3771434C00000578-3750855-image-a-22_1471731580217
Neymar do Santos amefanikiwa kuiongoza timu yake ya taifa kutwaa medali ya dhahabu ya kwanza katika historia ya mashindano ya Olympic kwa mchezo wa mpira wa miguu, ushindi huo dhidi ya Ujerumani utafsirika kama ni kisasi kwa kutokana na kuwahi kufungwa 7-1 miaka miwili iliyopita katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la dunia.
5114 - Copy
Brazil ambao wamewahi kutwaa mataji mengi ya soka wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa penati 5-4 hiyo ni baada ya mchezo kumalizika katika muda wa kawaida wakiwa sare ya goli 1-1, magoli ambayo yalifungwa na Neymar dakika ya 26 na kwa upande wa Ujerumani Max Meyer dakika ya 59, Brazil wamewahi kuikosa medali ya dhahabu ya Olympic katika vipindi vitano tofauti.
37720FE000000578-3750855-image-a-63_1471738393733

Jumamosi, 13 Agosti 2016

MESSI ATANGAZA KUREJEA KWENYE KIKOSI ARGENTINA

Agosti 13, 2016 0

Habari nzuri kwa raia wapenda soka nchini Argentina na mashabiki wa timu ya FC Barcelona ni kwamba anayetajwa kuwa mchezaji ambaye hajawahji kutokea wa aina yake katika historia ya mchezo wa soka Lionel Messi kutangaza rasmi kuwa anarudi kukitumikia tena kikosi cha timu ya taifa lake.
Aliitangazia Dunia maamuzi yake hayo magumu ya kusitisha kuichezea timu yake ya taifa mapema baada ya timu hiyo kushindwa kutwaa ubingwa wa Copa America mnamo tarehe 27 ya mwezi June mwaka huu ambapo timu hiyo ilijikuta inalazwa na viatu baada ya kufungwa katika mikwaju ya penalty kwa jumla ya penalty 4-2 na timu ya taifa ya Chile.
Ijumaa August 12 mkali huyo wa kucheka na nyavu ameitangazia tena dunia kutaka kurejea katika kikosi cha timu ya taifa lake.
Ni upendo tu wa taifa lake ndio umemsukuma Lionel Messi kubadilisha mawazo yake, ukiachilia mbali kiapo alicho kula mbele ya umma. Ikiwa ni kwa mujibu wa Sky Sport.

Muethiopia Ayana atwaa dhahabu na rekodi Rio

Agosti 13, 2016 0

Raia wa Ethiopia Almaz Ayana ameishindia Afrika dhahabu ya kwanza Michezo ya Olimpiki mjini Rio na kuvunja rekodi ya dunia mbio za mita 10000 wanawake.
Ayana aliwaacha nyuma wapinzani wake mbio zikiwa katikati na kuendelea hadi mwisho, muda wake ukiwa dakika 29 sekunde 17.45.
Rekodi ya awali iliwa 29:31.78 na iliwekwa na Mchina Wang Junxia mwaka 1993. Mkenya Vivian Cheruiyot ameshinda fedha naye raia mwingine wa Ethiopia Tirunesh Dibaba akachukua shaba.

Ijumaa, 12 Agosti 2016

Usitegemee kumuona Pogba akiichezea Man United weekend hii, kafungiwa

Agosti 12, 2016 0

Najua inawezekana wewe ni mmoja kati ya mashabiki wa soka duniani wanaosubiri kumuona staa wa kimataifa wa Ufaransaaliyejiunga na Man United akitokea Juventusya Italia Paul Pogba akiichezea Man Unitedkatika mchezo wa ufunguzi wa Man Uniteddhidi ya Bournemouth weekend hii.

Stori kutoka chama cha soka cha England FAkimethibitisha staa huyo kufungiwa kucheza mechi ya ufunguzi kutokana na kuwa na adhabu ya kadi mbili za njano alizooneshwa katika michuano ya Copa Italia akiwa naJuventus ya Italia, adhabu ambayo kwa mujibu wa kanuni anahama nayo.
Paul-Pogba-competes-with-Alessandro-Florenzi
Paul Pogba alijiunga na Man United akitokea Juventus ya Italia kwa ada ya uhamisho wa rekodi ya dunia wa pound milioni zaidi ya 100, lakini Paul Pogba anaungana na Robert Huth,Moussa Dembele na Chris Smalling waliofungiwa na FA kucheza mechi za ufunguzi.

Jumatatu, 8 Agosti 2016

Pogba kufanyiwa vipimo vya afya Manchester United

Agosti 08, 2016 0
Klabu ya Juventus ya Italia imemruhusu mshambulizi wake Paul Pogba kufanyiwa vipimo vya afya Old Trafford katika moja ya ishara kuwa huenda Manchester United imeafikiana na wakala wake kumnunua mchezaji huyo.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa amekuwa likizoni Marekani baada ya kumalizika kwa michuano ya Euro 2016.
Pogba, 23, amekuwa akihusishwa na kuhamia Old Trafford kwa bei ya kuvunja rekodi ya dunia ya ununuzi wa wachezaji ya pauni milioni moja.
Pogba alichezea United mwisho dhidi ya Wolves Machi 2012
Akiwa Old Trafford Pogba alichezeshwa katika mechi 3 pekee.
Meneja wa United Jose Mourinho alikuwa amedokeza kwamba klabu hiyo ilikuwa imekaribia sana kumpata Pogba.
"Kwa sasa, Pogba ni mchezaji wa Juventus," amesema Allegri.
United wameanza msimu kwa ushindi wa mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Leicester City Jumapili.
Juventus wataanza msimu wao Serie A wiki moja baadaye tarehe 20 Agosti.

Alhamisi, 4 Agosti 2016

Mwenge wa Olimpiki wawasili Rio de Janeiro,Brazil

Agosti 04, 2016 0

Mwenge wa Olimpiki umefika katika mji wa Rio de Janeiro kwa kutumia usafiri wa boti baada ya ziara ya muda wa miezi mitatu kuzunguuka miji mikubwa ya Brazil.

Meya wa mji wa Rio, Eduardo Paes, ndiye aliyeubeba mwenge huo wa Olimpiki miongoni mwa watu wachache waliofanikiwa kuushika.

Safari hiyo ya miezi mitatu haikuwa rahisi kwani kuna wakati msafara wa mwenge huo wa Olimpiki ulipokuwa ukipitishwa ulikumbana na waandamanaji wenye hasira kali kuhusiana na suala la gharama kubwa zilizotumika mpaka kuwa wenyeji wa michuano hiyo maarufu ulimwenguni.

Polisi wa kutuliza ghasia iliwalazimu kutumia mabomu ya machozi na pilipili za kupuliza ili kuwatawanya waandamanaji hao wenye hasira.

Kwa sasa nchi ya Brazil inapita katika kipindi cha mpito wa hali mbaya ni katika mtego wa anguko kubwa la kiutawala na mgogoro wa kisiasa, na maandamano zaidi yanatarajiwa siku ya ufunguzi wa michuano hiyo ya Olimpiki inayotarajiwa siku ya Ijumaa.
Waandaaji wa michuano hiyo wameonesha masikitiko yao makubwa kutokana na mwitikio mdogo ulooneshwa na wabrazil kwani tiketi zaidi ya milioni moja bado hazijanunuliwa huku sherehe za ufunguzi zimekaribia.

Jumatatu, 18 Julai 2016

List na picha za washindi wa tuzo 13 za Ligi Kuu Tanzania bara 2015/2016

Julai 18, 2016 0

Usiku wa July 17 2016 kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom ambayo ndio wadhamini wakuu wa Ligi Kuu soka Tanzaniabara, walitangaza na kutoa tuzo 13 kwa wachezaji, refa na timu bora zilizofanya vizuri msimu wa 2015/2016,  Vodacom kwa kushirikiana na TFF wamefanikiwa kuchagua na kutoa zawadi kwa washindi wa tuzo hizo.
DSC_1657
Washindi wa tuzo Ligi Kuu katika picha ya pamoja na wageni waalikwa
List ya washindi wa tuzo na zawadi walizochukua
  • Mchezaji bora wa Ligi Kuu 2015/2016 niJuma Abdul wa Yanga Tsh Milioni 9,228,820
  • Mchezaji bora wa kigeni ni Thabani Kamusoko wa Yanga Tsh Milioni 5,742,940
  • Mfungaji bora ni Amissi Tambwe waYanga Tsh Milioni 5,742,940
  • Mchezaji bora chipukizi ni Mohamed Hussein wa Simba Tsh Milioni 4.
  • Golikipa bora ni Aishi Manula wa Azam FC Tsh Milioni 5,742,940
  • Refa bora ni Ngole Mwangole Tsh Milioni 5,742,940
  • Kocha bora ni Hans van Pluijm waYanga Tsh Milioni 8.
  • Timu yenye nidhamu Mtibwa Sugar Tsh Milioni 17,228,820
  • Bingwa wa Ligi Kuu Yanga Tsh Milioni 81,345,723
  • Mshindi wa pili Azam FC Tsh Milioni 40,672,861
  • Mshindi wa tatu Simba Tsh Milioni 29,052,044
  • Mshindi wa nne Tanzania Prisons Tsh Milioni 23, 241,635
  • Mfungaji wa goli bora ni Ibrahim Ajib waSimba Tsh Milioni 3
DSC_1532
Kocha wa Yanga Hans van Pluijm baada ya kutwaa tuzo ya kocha bora akisalimiana na waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba
DSC_1521
Kocha wa Yanga Hans van Pluijm akipokea tuzo ya kocha bora akiwa kaongozana na mkewe.
DSC_1536
Kocha wa Yanga Hans van Pluijm akisalimiana na Rais wa TFF Jamal Malinzi
DSC_1542
Mwameja akikabidhi tuzo ya golikipa bora kwa Aishi Manula wa Azam FC
DSC_1550 - Copy
Ibrahim Ajib akipokea mfano wa hundi ya Tsh Milioni 3 kama zawadi ya ufungaji goli bora.
DSC_1560
Thabani Kamusoko akiwa na mkewe na mtoto wake alipopokea mfano wa hundi ya Tsh Milioni 5 kama zawadi ya mchezaji bora wa kigeni.
DSC_1584
Kutoka kushoto ni Mohamed Hussein wa Simba ambaye ameshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi.
DSC_1604
Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba akimkabidhi tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu Juma Abdul wa Yanga
DSC_1650
Kutoka kushoto ni mkuu wa masoko wa Yanga Omar, Juma Abdul na golikipa wa Yanga Deogratus Munish
DSC_1678
DSC_1690
DSC_1757
DSC_1386
DSC_1388
DSC_1395
DSC_1403
DSC_1417
DSC_1423
Kamusoko na familia yake
DSC_1430 - Copy