.

Jumamosi, 13 Agosti 2016

MESSI ATANGAZA KUREJEA KWENYE KIKOSI ARGENTINA


Habari nzuri kwa raia wapenda soka nchini Argentina na mashabiki wa timu ya FC Barcelona ni kwamba anayetajwa kuwa mchezaji ambaye hajawahji kutokea wa aina yake katika historia ya mchezo wa soka Lionel Messi kutangaza rasmi kuwa anarudi kukitumikia tena kikosi cha timu ya taifa lake.
Aliitangazia Dunia maamuzi yake hayo magumu ya kusitisha kuichezea timu yake ya taifa mapema baada ya timu hiyo kushindwa kutwaa ubingwa wa Copa America mnamo tarehe 27 ya mwezi June mwaka huu ambapo timu hiyo ilijikuta inalazwa na viatu baada ya kufungwa katika mikwaju ya penalty kwa jumla ya penalty 4-2 na timu ya taifa ya Chile.
Ijumaa August 12 mkali huyo wa kucheka na nyavu ameitangazia tena dunia kutaka kurejea katika kikosi cha timu ya taifa lake.
Ni upendo tu wa taifa lake ndio umemsukuma Lionel Messi kubadilisha mawazo yake, ukiachilia mbali kiapo alicho kula mbele ya umma. Ikiwa ni kwa mujibu wa Sky Sport.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni