.

Ijumaa, 12 Agosti 2016

Usitegemee kumuona Pogba akiichezea Man United weekend hii, kafungiwa


Najua inawezekana wewe ni mmoja kati ya mashabiki wa soka duniani wanaosubiri kumuona staa wa kimataifa wa Ufaransaaliyejiunga na Man United akitokea Juventusya Italia Paul Pogba akiichezea Man Unitedkatika mchezo wa ufunguzi wa Man Uniteddhidi ya Bournemouth weekend hii.

Stori kutoka chama cha soka cha England FAkimethibitisha staa huyo kufungiwa kucheza mechi ya ufunguzi kutokana na kuwa na adhabu ya kadi mbili za njano alizooneshwa katika michuano ya Copa Italia akiwa naJuventus ya Italia, adhabu ambayo kwa mujibu wa kanuni anahama nayo.
Paul-Pogba-competes-with-Alessandro-Florenzi
Paul Pogba alijiunga na Man United akitokea Juventus ya Italia kwa ada ya uhamisho wa rekodi ya dunia wa pound milioni zaidi ya 100, lakini Paul Pogba anaungana na Robert Huth,Moussa Dembele na Chris Smalling waliofungiwa na FA kucheza mechi za ufunguzi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni