.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Celebrities. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Celebrities. Onyesha machapisho yote

Jumanne, 11 Julai 2017

21 Savage Akanusha Kununuliwa Gari Na Drake

Julai 11, 2017 0

Rapa 21 Savage amezima stori kuwa alinunuliwa gari ya kifahari aina ya Ferrari na Drake kwaajili ya Birthday yake.
Savage anasema ”Drake alinipa gari aina ya Ferrari nitumie tu wakati nikiwa L.A kwaajili ya Birthday yangu ila lilikuwa la kuazimwa, baadae nilipenda gari kama hio ndio nikanunua Ferrari yake” 
Savage amemsifia Drake kwa kuwa mtu powa kwake kutokana na kumjali na kukumbuka kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa tofauti na wasanii wengine wa rapa.
21 Savage alitoa album mpya July 7 Issa Album.
 

Baraka The Prince Akanusha Kusimamiwa Na Ali Kiba

Julai 11, 2017 0

Msanii Baraka The Prince ambaye yupo chini ya usimamizi wa kampuni ya RockStar4000 amefunguka na kusema kuwa yeye ni msanii aliye chini ya usimamizi wa RockStar4000 na si msanii aliye chini ya Alikiba. 


Baraka The Prince amesema hayo kupitia kipindi cha 5 Selekt na kusema yeye anatambua kuwa Alikiba sasa amekuwa Director wa kampuni hiyo na anaamini anaweza kufanya vizuri lakini yeye hana taarifa zozote juu ya mchongo huo ambao ameupata Alikiba kwenye uongozii wake huo. 

"Mimi sitaki sana kuzungumzia sana juu ya Alikiba kuwa Director wa RockStar4000 kwani kipindi ambacho yeye anaingia mikataba mimi nilikuwa Nairobi na wao walikuwa Afrika Kusini na sijapata nafasi kusikia chochote hivyo kwa sasa bado sijui vizuri hilo jambo, siwezi kulizungumzia japo nafahamu maana naweza kuzungumzia nikazungumza nikasema jambo lisilo la kweli. Ila nimefurahi sababu Alikiba ni kaka yangu na naishi naye vizuri na najua kuwa kazi itakwenda vizuri". Amesema 

Mbali na hilo Baraka The Prince alitoa ufafanuzi kuwa yeye ni msanii anayesimamiwa kazi zake na kampuni ya RockStar4000 na si kusimamiwa na Alikiba kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakidhani au wakihisi hivyo. 

"Mimi ni msanii wa RockStar4000 na si msanii wa Alikiba hilo watu naomba waelewe" alisema Baraka The Prince 

Kwa kumalizia Baraka The Prince alisema watu wengi wanamchukia kutokana na misimamo yake katika kazi yake ya muziki na kudai wasanii wengi wa bongo wamekuwa wakifanya kazi zao kienyeji sana ndiyo maana anapishana nao, kwani yeye anataka kazi ambayo anashiriki iweze kuwekewa mipango na iende katika viwango.

Lil Kim Kuua Bif Kati Ya Remy Ma na Nicki Minaj

Julai 11, 2017 0

Rapa wa kike kutoka Marekani Lil Kim katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa leo anakumbukwa kwa maneno yake ya kujiweka mbali na bifu kubwa linalo fuatiliwa sana na watu wengi nchini Marekani kwa hasa katika muziki wa Rap/Hip Hop kwa upande wa wakina mama.
Related image
Bifu la Nicki Minaj na Remy Ma lilizidi kuwa kubwa baada ya Remy Ma kutwaa tuzo ya BET BEST FEMALE RAPPER  lakini licha ya bifu lao kuwa kubwa Lil Kim alishasikika katika mahojiano na kituo cha Billboard kuhusu Bifu hilo na kusema kuwa hana mpango wa kuungana na Remy Ma kumdiss Nicki Minaj.

Image result for nicki minaj


Lil Kim ambaye alishamdiss NickiMinaj kupitia ngoma ya ‘Black Friday’ aliongeza kuwa hana bifu kabisa na Nicki kwakuwa walishamaliza na kikubwa ambacho anaweza kusema kuhusu marapa hao wa kike ni kuwa shirikisha wote wawili katika album yake mpya.

Sababu Za Wema Sepetu Kutokutokea Katika Video Ya Haitham

Julai 11, 2017 0
Msanii wa Bongo Fleva, Haitham amefafanua sababu ya Wema Sepetu kutoonekana katika video ya ngoma yake mpya ‘Play Boy’ ambayo amemshirikisha mrembo huyo. 



Haitham amesema kulikuwa na mipango ya kufanya video na Wema na script ilikuwa tayari imeshaandikwa ila alipokosekana ilibidi wabadilishe. 

“Na script ambayo tumefanya sasa inayoonekana kwenye video wasichana watatu ilibadilishwa fasta baada ya Wema kutokutokea kwenye video, so script ya mwanzo ambayo Wema alipaswa kuwepo aliandika yeye director na baada ya mabadiliko kutokea akabadilisha scrip,” ameiambia E-News ya EATV. 

Kuhusu athari zilizojitokeza baada ya Wema kutokuwepo kwenye video,  amesema “kwa upande wingine yameathiri kidogo sio sana kwa sababu kuna baadhi ya mashabiki wa Wema walitamani kumuona kwenye video, kwa hiyo ameathiri kidogo kwa wale mashabiki walikuwa wanatamani kumuona,” amesisitiza. 

Play Boy ni ngoma ya pili kwa Wema Sepetu kushirikishwa na msanii wa Bongo Flava baada ya ile ya mwanzo ‘Shoga Yake Mama’ aliyopewa shavu na Snura, lakini hizo zote hakuna hata moja Wema ametokea kwenye video.

Juma Nature Azungumzia Ishu Ya Ndala Zake Kubuma

Julai 11, 2017 0
Juma Nature Azungumzia Ishu Ya Ndala Zake Kubuma
Msanii mkongwe wa Bongo Flava, Juma Nature ameeleza ni kwa nini hadi sasa bidhaa zake za ndala hazijaingia sokoni.
Hapo awali msanii huyo alijidai kuwa angekuja na bidhaa hizo lakini hadi sasa hakuna alichotekeleza. Akizungumza na Planet Bongo ya EA Radio amesema ameamua kusitisha mpango huo.
“Unajua kila jambo ukilianzisha watu wengine wanaangalia ulichosema wewe ndio wanakaa wakifanye, hivyo nikaamua niache,” amesema Juma Nature.
Baadhi ya wasanii wamekuwa wakiingiza bidhaa zao sokoni, Weusi wameuza t-shirt, pensi na kufia kupitia brand yao ya Nyeusi, Jux amefanya hivyo kupitia brand yake ya African Boy na Diamond ameingiza bidhaa mbali mbali ikiwepo Chibu Perfume.

Rihanna Kungaa Kwenye Maonyesho Ya Mitindi

Julai 11, 2017 0
Rihanna Kungaa Kwenye Maonyesho Ya Mitindi


Mwanamuziki Rihanna anatarajia kushiriki katika onyesho  la mavazi  New York Fashion Week -Marekani, akiwa na bidhaa yake ya Fenty Puma aliyoizindua mwaka juzi. Katika onyesho hilo Rihanna anatarajiwa kuonyesha mavazi yatakayotumika kipindi cha mwaka 2018.
“After two successful seasons showing during Paris Fashion Week, Rihanna has decided to return to New York and show her Fenty Puma by Rihanna spring 2018 collection during NYFW, making this the first time she will present during September NYFW,” wamesema Puma.
Hii ni mara ya kwanza kwa msanii huyo kuonyesha mavazi yake katika wiki ya mitindo tangu alipozindua mwaka 2016 katika NYFW kabla ya kuzipeleka Paris Fashion Week kuzindua msimu wa mavazi hayo kwa mwaka 2017.

Jumamosi, 8 Julai 2017

Wizkid Afanya Maajabu Katika Album Yake Mpya

Julai 08, 2017 0

Msanii kutoka Nigeria Wizkid anategemea kutoa album yake mpya mwezi huu iliyopewa jina Sounds From the Other Side.
CD hii inatoka July 14, kupitia Starboy/RCA/Sony Music International, ikiwa na colabo ya DrakeMajor Lazer, Chris BrownTy Dolla $ignBucie & Trey Songz.
Ty Dolla $ign
Bucie
Chris Brown
Drake
Trey Songz
SOUNDS FROM THE OTHER SIDE TRACKLISTING

1. “Sweet Love”
2. “Come Closer” feat. Drake
3. “Naughty Ride” feat. Major Lazer
4. “African Bad Gyal” feat. Chris Brown
5. “Daddy Yo”
6. “One For Me” feat. Ty Dolla $ign
7. “Picture Perfect”
8. “Nobody”
9. “Sexy”
10. “All For Love” feat. Bucie
11. “Dirty Wine” feat. Ty Dolla $ign
12. “Gbese” feat. Trey Songz

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka HabNews Tv

Bonyeza HAPA kupakua application yetu na upate habari punde zitufikiapo

Jumanne, 4 Julai 2017

Rihanna Aonekana Wa Furaha Kwa Mpenzi Wake Mpya

Julai 04, 2017 0
 
Rihanna anatabasamu mpaka jino la mwisho sasa baada ya kugundulika kuwa mpenzi wake mpya Hassan Jameel anampa raha kuliko alivyowahi kufanya Drake.
Rihanna, 29, alikutana na billionaire Hassan nchini Spain, na toka muda huo wawili hawa hawatengani, kutokana na penzi lao zito na mkwanja mrefu anaomiliki Hassan tofauti kabisa na Ma Ex wake kama Chris Brown na Drake.
Mapaparazzi wa Ibiza wanasema Hassan anamuheshimu sana Rihanna kitu kinachomfana staa huyu wa RnB asibanduke hapo. #MoneyPowerRespect
Rihanna amekuwa na mahusiano na watu maarufu toka mwaka 2007 alivyokuwa na mwigizaji Shia LaBeouf , Chris Brown, Drake, mcheza baseball maarufu Matt Kemp, mwigizaji Leonardo DiCaprio, rapa Travi$ Scott, na sasa Bilionea Hassan Jemeel .
  

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka HabNews Tv

Bonyeza HAPA kupakua application yetu na upate habari punde zitufikiapo

Chin Bees Atakiwa Kubadili Jina

Julai 04, 2017 0


Msanii wa hip hop Bongo, Chid Benz amemtaka msanii mwenzake Chin Bees kutafuta jina lingine.
Sababu ya Chid Benz kusema hivyo imetokana na majina yao kufanana, na kuongeza kuwa wote wanafanya muziki wa aina tofauti hivyo kulikuwa hakuna ulazima wa ufanya hivyo.
“Siku moja nimeona Shetta anamuangalia instagram nikamuuliza huyo ni nini?, akaniambia ni Chin Bees, nikamuuliza anafanya muziki gani, akaniambia Bongo Fleva!. Sisemi kwa ubaya ila sikuelewa ile style anayofanya yeye ni tofauti sana na mimi mtu mzima mwenye hit kama 32 najua nikiingia kwenye stage nachapa tu,” Chid Benz ameiambia Planet Bongo ya EA Radio na kuhoji.
“Huyo Chin Bees ana single hata saba kweli?, atafute jina lingine,” amemaliza kwa kusema.

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka HabNews Tv

Bonyeza HAPA kupakua application yetu na upate habari punde zitufikiapo

Jumatatu, 3 Julai 2017

Kanye West Ajitoa Kwenye Mtandao Wa TIDAL Wa Jay-Z

Julai 03, 2017 0

Msanii wa hiphop nchini Marekani Kanye West amejitoa kwenye mtandao wa TIDAL wa Jay-Z kisa kikitajwa kuwa ni maslahi ya kifedha.
Kwa mujibu wa TMZ, Kanye alikuwa kiungo muhimu ndani ya mtandao huo wa kutazama na kusikiliza kazi za muziki, TIDAL ilipata wateja wengi zaidi baada ya album ya Kanye West SAINT PABLO kutoka kupita mtandao huo.
Sababu za kujitoa zimetajwa kuwa ni kushindwa kuelewana kwenye masuala ya malipo na kampuni ya TIDAL na maneno makali ya Jay Z kwa Kanye West kwenye album yake mpya ya 4:44.
Wanasheria wa pande zote mbili wanajipanga kwenda mahakamani. Inasemekana Kanye amekuwa akilalamika kuwa anawadai TIDAL dola milioni 3.

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka HabNews Tv

Bonyeza HAPA kupakua application yetu na upate habari punde zitufikiapo

Idris Sultan apata shavu Hollywood

Julai 03, 2017 0


Baada ya wiki ya mchakato wa usahili, Mshindi wa Big Brother Africa-Hotshots wa 2014, Idris Sultan ataonekana katika filamu ya ‘Ballin …On the Other Side of the World,’ itayoandaliwa nchini Marekani chini ya muongozaji Harvey White.
Muongozaji wa filamu hiyo aliwahi kufanya kazi na wasanii wenye majina makubwa akiwemo Chris Brown, Mariah Carey, Lady Gaga na Tamia.
Akiwa kama mhariri wa filamu, amehariri baadhi ya filamu kama vile ‘Think Like A Man 2,’ ‘The Wedding Ringer,’ na ‘King of the Dance Hall’ akishirikiana na Whoopi Goldberg.
Hadithi ya filamu hiyo imetungwa na Torino Von Jones, ambapo hadithi hiyo inamhusu kijana mdogo wa Kenya (Kunjani), ambaye wazazi wake ni waathirika wa uhalifu uliojaa vurugu.
Siku moja katika maeneo ya ya shule, kijana huyo aliye na umri wa miaka kumi na tatu aligunduliwa na padri wa Kimarekani ambaye alimwona akicheza mpira wa kikapu na akaamini ana uwezo mkubwa na anaweza kushirikia ligi ya NBA.
Wote wawili waliendelea na urafiki wao na padri huyo alianza kumpatia ushauri. (King) itaigizwa na  Sultan, ana haiba kubwa,lakini ni mhalifu mkubwa na hatari sana ambaye ana wazo jingine na anataka Kunjani kujiunga na kundi lake la wahalifu na atafanya kila liwezekanalo ili mpango huo ufanikiwe.
Mara ya mwisho Sultan alionekana katika filamu ya Tanzania ‘Kiumeni,’ ambayo itaoneshwa katika tamasha lijalo la wiki ya filamu la Zanzibar (ZIFF)  ambapo ‘Kiumeni’ itaoneshwa wakati wa Siku ya tamasha ya filamu za Kiswahili ya ZIFF Julai 14, na mtayarishaji na nyota wa filamu  Ernest Napoleon.
Mapema mwaka huu, Napoleon aliweka historia wakati alipochaguliwa kuwa  rais wa kampuni ya uzalishaji na usambazaji wa filamu ya Marekani ya  D Street Media Group yenye makao yake jijini New York, pamoja na ofisi katika miji ya Berlin, Buenos Aires na Cape Town.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa D Street na mtayarishaji mtendaji Dexter Davis walimtambua Idris kutokana na kuiangalia  filamu ya “Kiumeni’.
“Idris Sultan has what it takes to become an international star and our upcoming film ‘Ballin… On the Other Side of the World’ is a perfect fit. We’re considering Mr. Sultan for other movies as well, alisema Davis.
Kampuni hiyo ya filamu inaazimia kupiga picha  sehemu za Marekani na Kenya na haitachelea kutafuta vipaji vingine kwa waigizaji  wa Kenya  na nchi nyingine za Afrika Mashariki  ikiwemo Tanzania pale inapolazimu.
Filamu hiyo imeandaliwa kwa bajeti ya Dola za Marekani milioni tano.

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka HabNews Tv

Bonyeza HAPA kupakua application yetu na upate habari punde zitufikiapo

Jumapili, 2 Julai 2017

Harry Kane Amvalisha Pete Mpenzi Wake

Julai 02, 2017 0


Mshambuliaji wa klabu ya Tottenham Hotspur, Harry Kane amemvalisha pete ya uchumba mpenzi wake Katie Goodland ambaye wana mtoto mmoja Ivy Jane.
Kane na Katie Goodland wamekuwa marafiki toka utotoni na jambo hili kubwa limetokea kwenye visiwa vya Nassau huko Bahamas.



Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka HabNews Tv

Bonyeza HAPA kupakua application yetu na upate habari punde zitufikiapo

Ijumaa, 30 Juni 2017

Rammy Atuletea Mgambia Baada Ya AGNESS Masogange Kumtema

Juni 30, 2017 0
STAA wa filamu Bongo, Rammy Gallis amenasa kifaa kipya kutoka nchini Gambia ambaye naye ni msanii wa filamu, Princess Shyngle na kusema kuwa mwanadada huyo ndiye anayemkonga nyoyo kwa sasa japo hapendi kumuuzisha sura. 
Akipiga stori na Star Mix baada ya meseji za mapenzi akichati na mwanadada huyo kunaswa na paparazi wetu, msanii huyo alifunguka kuwa, yupo kwenye uhusiano na mlimbwende huyo kwa muda sasa na kwamba miongoni mwa vitu vilivyomvutia kwake ni pamoja na figa matata aliyonayo.


“Nilikutana na Princess nilipoenda kufanya filamu Nigeria, kwa kuwa yeye ni Mgambia lakini makazi yake makubwa ni Nigeria, nampenda sana naamini yeye ndiye tulizo la moyo wangu, mapenzi ya Kibongo yanitue kwa sasa,” alisema.

 Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka HabNews Tv

Bonyeza HAPA kupakua application yetu na upate habari punde zitufikiapo

Alhamisi, 29 Juni 2017

Fast And Furious Kumkosa Star Huyu

Juni 29, 2017 0


Mwigizaji maarufu HollyWood Michelle Rodriguez ametishia kuaga filamu za Fast & Furious kupitia IG yake huku mashabiki wakimwaga comment za kumuomba asiondoke.
Michelle Rodriguez amekuwa na filamu hizi toka mwazo wa The Fast & the Furious, ila kuna tetesi kuwa anaweza asirudi tena kwenye toleo la 9 na 10.
Michelle Rodriguez  aliandika hivi kwenye IG yake “F8 is out digitally today, I hope they decide to show some love to the women of the franchise on the next one. Or I just might have to say goodbye to a loved franchise,It’s been a good ride & Im grateful for the opportunity the fans & studio have provided over the years… One Love.” Akimaanisha >> F8 imetoka digitally leo, nategemea watatuonyesha mapenzi zaidi waigizaji wa kike kwenye toleo lijalo lasivyo nitabidi niache filamu inayopendwa zaidi, nashukuru kwa nafasi niliyopewa na studio hii, mashabiki, One Love

Fast & the Furious 9 na 10 zimesha dhibitishwa kutolewa April 19, 2019, na F10 itatoka April 2, 2021.

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka HabNews Tv

Bonyeza HAPA kupakua application yetu na upate habari punde zitufikiapo

Witness Adai Mapenzi Huchangia Kupunguza Unene

Juni 29, 2017 0


Msanii wa Bongo Fleva, Witnes a.k.a Kibonge Mwepesi amesema kufanya mapenzi kunapunguza unene.
Muimbaji huyo wa zamani wa kundi la Wakilisha ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa kuna vitu vingi ambavyo hupelekea mtu kupungua unene lakini ufanyaji wa mapenzi walau mara tatu kwa wiki kunasaidia.
“Lakini unatakiwa kujua kwa wiki unafanya mapenzi mara ngapi. Ni vema si chini ya mara tatu kwa hiyo kwa mwezi mara 12 lakini ukiweza kuzidisha zaidi ni fresh,” amesema Witnes.

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka HabNews Tv

Bonyeza HAPA kupakua application yetu na upate habari punde zitufikiapo

Alhamisi, 22 Juni 2017

Bei Za Ticket Ya Pambano La Floyd Mayweather Vs Conor McGregor Zatajwa

Juni 22, 2017 0
Bei za Ticket za pambano la Floyd Mayweather Vs Conor McGregor zimetoka,Ticket ya bei ndogo zaidi ni dola $2, 013 ‘Milioni 4,505,094 za Tanzania.
Pambano hili limetajwa kuwa pambano lenye dhamani ya dola bilioni moja, “The Billion Dollar Fight,” litakalo fanyika mjini Las Vegas.
Bei za ticket za pambano hili la Mayweather Vs McGregor zimeanza kwanzia kiti cha dola $2, 013, kuna ticket za dola $59,377 ambayo ni milioni 132,873,850 ya TZ, na mpaka zile za dola $93,609 ambayo ni Milioni 209,478,220.
Ripoti inasema Pay-Per itaingiza zaidi ya dola milioni 4.4 ikiwa ni rekodi iliyowekwa na pambano la Mayweather vs. Pacquiao

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka HabNews Tv

Bonyeza HAPA kupakua application yetu na upate habari punde zitufikiapo