.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Music. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Music. Onyesha machapisho yote

Jumanne, 11 Julai 2017

21 Savage Akanusha Kununuliwa Gari Na Drake

Julai 11, 2017 0

Rapa 21 Savage amezima stori kuwa alinunuliwa gari ya kifahari aina ya Ferrari na Drake kwaajili ya Birthday yake.
Savage anasema ”Drake alinipa gari aina ya Ferrari nitumie tu wakati nikiwa L.A kwaajili ya Birthday yangu ila lilikuwa la kuazimwa, baadae nilipenda gari kama hio ndio nikanunua Ferrari yake” 
Savage amemsifia Drake kwa kuwa mtu powa kwake kutokana na kumjali na kukumbuka kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa tofauti na wasanii wengine wa rapa.
21 Savage alitoa album mpya July 7 Issa Album.
 

Baraka The Prince Akanusha Kusimamiwa Na Ali Kiba

Julai 11, 2017 0

Msanii Baraka The Prince ambaye yupo chini ya usimamizi wa kampuni ya RockStar4000 amefunguka na kusema kuwa yeye ni msanii aliye chini ya usimamizi wa RockStar4000 na si msanii aliye chini ya Alikiba. 


Baraka The Prince amesema hayo kupitia kipindi cha 5 Selekt na kusema yeye anatambua kuwa Alikiba sasa amekuwa Director wa kampuni hiyo na anaamini anaweza kufanya vizuri lakini yeye hana taarifa zozote juu ya mchongo huo ambao ameupata Alikiba kwenye uongozii wake huo. 

"Mimi sitaki sana kuzungumzia sana juu ya Alikiba kuwa Director wa RockStar4000 kwani kipindi ambacho yeye anaingia mikataba mimi nilikuwa Nairobi na wao walikuwa Afrika Kusini na sijapata nafasi kusikia chochote hivyo kwa sasa bado sijui vizuri hilo jambo, siwezi kulizungumzia japo nafahamu maana naweza kuzungumzia nikazungumza nikasema jambo lisilo la kweli. Ila nimefurahi sababu Alikiba ni kaka yangu na naishi naye vizuri na najua kuwa kazi itakwenda vizuri". Amesema 

Mbali na hilo Baraka The Prince alitoa ufafanuzi kuwa yeye ni msanii anayesimamiwa kazi zake na kampuni ya RockStar4000 na si kusimamiwa na Alikiba kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakidhani au wakihisi hivyo. 

"Mimi ni msanii wa RockStar4000 na si msanii wa Alikiba hilo watu naomba waelewe" alisema Baraka The Prince 

Kwa kumalizia Baraka The Prince alisema watu wengi wanamchukia kutokana na misimamo yake katika kazi yake ya muziki na kudai wasanii wengi wa bongo wamekuwa wakifanya kazi zao kienyeji sana ndiyo maana anapishana nao, kwani yeye anataka kazi ambayo anashiriki iweze kuwekewa mipango na iende katika viwango.

Lil Kim Kuua Bif Kati Ya Remy Ma na Nicki Minaj

Julai 11, 2017 0

Rapa wa kike kutoka Marekani Lil Kim katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa leo anakumbukwa kwa maneno yake ya kujiweka mbali na bifu kubwa linalo fuatiliwa sana na watu wengi nchini Marekani kwa hasa katika muziki wa Rap/Hip Hop kwa upande wa wakina mama.
Related image
Bifu la Nicki Minaj na Remy Ma lilizidi kuwa kubwa baada ya Remy Ma kutwaa tuzo ya BET BEST FEMALE RAPPER  lakini licha ya bifu lao kuwa kubwa Lil Kim alishasikika katika mahojiano na kituo cha Billboard kuhusu Bifu hilo na kusema kuwa hana mpango wa kuungana na Remy Ma kumdiss Nicki Minaj.

Image result for nicki minaj


Lil Kim ambaye alishamdiss NickiMinaj kupitia ngoma ya ‘Black Friday’ aliongeza kuwa hana bifu kabisa na Nicki kwakuwa walishamaliza na kikubwa ambacho anaweza kusema kuhusu marapa hao wa kike ni kuwa shirikisha wote wawili katika album yake mpya.

Sababu Za Wema Sepetu Kutokutokea Katika Video Ya Haitham

Julai 11, 2017 0
Msanii wa Bongo Fleva, Haitham amefafanua sababu ya Wema Sepetu kutoonekana katika video ya ngoma yake mpya ‘Play Boy’ ambayo amemshirikisha mrembo huyo. 



Haitham amesema kulikuwa na mipango ya kufanya video na Wema na script ilikuwa tayari imeshaandikwa ila alipokosekana ilibidi wabadilishe. 

“Na script ambayo tumefanya sasa inayoonekana kwenye video wasichana watatu ilibadilishwa fasta baada ya Wema kutokutokea kwenye video, so script ya mwanzo ambayo Wema alipaswa kuwepo aliandika yeye director na baada ya mabadiliko kutokea akabadilisha scrip,” ameiambia E-News ya EATV. 

Kuhusu athari zilizojitokeza baada ya Wema kutokuwepo kwenye video,  amesema “kwa upande wingine yameathiri kidogo sio sana kwa sababu kuna baadhi ya mashabiki wa Wema walitamani kumuona kwenye video, kwa hiyo ameathiri kidogo kwa wale mashabiki walikuwa wanatamani kumuona,” amesisitiza. 

Play Boy ni ngoma ya pili kwa Wema Sepetu kushirikishwa na msanii wa Bongo Flava baada ya ile ya mwanzo ‘Shoga Yake Mama’ aliyopewa shavu na Snura, lakini hizo zote hakuna hata moja Wema ametokea kwenye video.

Jumamosi, 8 Julai 2017

Wizkid Afanya Maajabu Katika Album Yake Mpya

Julai 08, 2017 0

Msanii kutoka Nigeria Wizkid anategemea kutoa album yake mpya mwezi huu iliyopewa jina Sounds From the Other Side.
CD hii inatoka July 14, kupitia Starboy/RCA/Sony Music International, ikiwa na colabo ya DrakeMajor Lazer, Chris BrownTy Dolla $ignBucie & Trey Songz.
Ty Dolla $ign
Bucie
Chris Brown
Drake
Trey Songz
SOUNDS FROM THE OTHER SIDE TRACKLISTING

1. “Sweet Love”
2. “Come Closer” feat. Drake
3. “Naughty Ride” feat. Major Lazer
4. “African Bad Gyal” feat. Chris Brown
5. “Daddy Yo”
6. “One For Me” feat. Ty Dolla $ign
7. “Picture Perfect”
8. “Nobody”
9. “Sexy”
10. “All For Love” feat. Bucie
11. “Dirty Wine” feat. Ty Dolla $ign
12. “Gbese” feat. Trey Songz

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka HabNews Tv

Bonyeza HAPA kupakua application yetu na upate habari punde zitufikiapo

Jumanne, 4 Julai 2017

Chin Bees Atakiwa Kubadili Jina

Julai 04, 2017 0


Msanii wa hip hop Bongo, Chid Benz amemtaka msanii mwenzake Chin Bees kutafuta jina lingine.
Sababu ya Chid Benz kusema hivyo imetokana na majina yao kufanana, na kuongeza kuwa wote wanafanya muziki wa aina tofauti hivyo kulikuwa hakuna ulazima wa ufanya hivyo.
“Siku moja nimeona Shetta anamuangalia instagram nikamuuliza huyo ni nini?, akaniambia ni Chin Bees, nikamuuliza anafanya muziki gani, akaniambia Bongo Fleva!. Sisemi kwa ubaya ila sikuelewa ile style anayofanya yeye ni tofauti sana na mimi mtu mzima mwenye hit kama 32 najua nikiingia kwenye stage nachapa tu,” Chid Benz ameiambia Planet Bongo ya EA Radio na kuhoji.
“Huyo Chin Bees ana single hata saba kweli?, atafute jina lingine,” amemaliza kwa kusema.

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka HabNews Tv

Bonyeza HAPA kupakua application yetu na upate habari punde zitufikiapo

Jumatatu, 3 Julai 2017

Kanye West Ajitoa Kwenye Mtandao Wa TIDAL Wa Jay-Z

Julai 03, 2017 0

Msanii wa hiphop nchini Marekani Kanye West amejitoa kwenye mtandao wa TIDAL wa Jay-Z kisa kikitajwa kuwa ni maslahi ya kifedha.
Kwa mujibu wa TMZ, Kanye alikuwa kiungo muhimu ndani ya mtandao huo wa kutazama na kusikiliza kazi za muziki, TIDAL ilipata wateja wengi zaidi baada ya album ya Kanye West SAINT PABLO kutoka kupita mtandao huo.
Sababu za kujitoa zimetajwa kuwa ni kushindwa kuelewana kwenye masuala ya malipo na kampuni ya TIDAL na maneno makali ya Jay Z kwa Kanye West kwenye album yake mpya ya 4:44.
Wanasheria wa pande zote mbili wanajipanga kwenda mahakamani. Inasemekana Kanye amekuwa akilalamika kuwa anawadai TIDAL dola milioni 3.

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka HabNews Tv

Bonyeza HAPA kupakua application yetu na upate habari punde zitufikiapo

Jumatano, 21 Juni 2017

Msanii Prodigy Wa Kundi La Mobb Deep Afariki Dunia Las Vegas,

Juni 21, 2017 0

    Rapa wa kundi la Mobb Deep, Prodigy amefariki dunia mjini Las Vegas akiwa na umri wa miaka 42. Prodigy alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Sickle Cell Anemia toka utotoni.
Msemaji wake amethibitisha taarifa hizi nakusema Prodigy aliugua ghafla baada ya show ya kundi hilo Vegas na na kupelekwa hospitalini akisumbuliwa na Sickle Cell Anemia.
Madaktari na polisi wanaendelea na uchunguzi juu ya kilichosababisha kifo cha rapa huyu.
Prodigy alikuwa Las Vegas kwenye ziara ya Art of Rap na wasanii kama Ghostface KillahOnyxKRS-One, na Ice-T.
Prodigy na Havoc, waliunda kundi la Mobb Deep mjini New York miaka ya tisini na kuteka muziki kupitia rekodi zao kubwa kama “Quiet Storm” na “Shook Ones.”

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka HabNews Tv

Bonyeza HAPA kupakua application yetu na upate habari punde zitufikiapo

Nicki Minaj Asusia Tuzo Za BET

Juni 21, 2017 0

Rapa Nicki Minaj hatohudhuria tuzo za BET mwaka huu kutokana na kuwania tuzo mmoja na rapa Remy Ma ambaye ametajwa kuwa na asilimia kubwa ya kushinda tuzo hio.
Nicki Minaj atakuwa na show ya kufanya kwenye tuzo za NBA siku mmoja baada ya tuzo za BET mwaka huu.
Kwenye kipengele hicho cha msanii bora wa HipHop wa Kike yupo Nick

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka HabNews Tv

Bonyeza HAPA kupakua application yetu na upate habari punde zitufikiapo

Ney Wa Mitego Asusia Album

Juni 21, 2017 0


Msanii wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego ameeleza ni kwanini hatoi albamu huku akitaja mitandao ni moja ya sababu.
Rapper huyo amesema kumekuwa na wizi mkubwa katika mtandao kitu ambacho kinapelekea msanii akitoa albamu haimnufaishi.
“Umeona mfano wa wasanii wawili watatu ambao wamejaribu kutoa albamu hapa katikati hazina faida kwa sababu unatoa albamu ikishaenda kwenye mtandao kila mtu anaenda ku-burn,” Nay ameiambia Radio One.
“Wengine wanaweka kwenye YouTube channel zao, wengine wanaweka kwenye mitandao yao ambayo ukiingia haulipii chochote. Mwisho wa siku unakuta ananunua mtu nmoja au wiwili, watatu lakini zaidi ya watu 1,000 wanaenda kuipata hiyo albamu bure,” ameongeza.

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka HabNews Tv

Bonyeza HAPA kupakua application yetu na upate habari punde zitufikiapo

Jumapili, 30 Aprili 2017

Tarajia Kolabo Hizi Kutoka Kwa Rayvan

Aprili 30, 2017 0
Tarajia Kolabo Hizi Kutoka Kwa Rayvan
Msanii Rayvanny ametaja kolabo zake na wasanii wa nje ambazo zipo tayari.
Muimbaji huyo, ambaye yupo nchini Sweden kwa ziara yake ya muziki, amemuambia mmoja wa watangazaji wa nchi hiyo kua, tayari ameshafanya kolabo na msanii mkubwa kutoka Nigeria, Afrika Kusini na Kenya.
“Nina kolabo na msanii mkubwa kutoka Nigeria, ingawa kwa sasa siwezi kutaja jina lake. Lakini pia kuna kolabo Afrika Kusini, na Kenya ukiacha Bahati, kuna mwingine Khaligraph Jones kutoka Nairobi,” amesema Ray.
Kwa msanii wa Afrika Kusini tayari muimbaji huyo kutoka WCB ameshafanya kolabo na Dj Maphorisa tangu mwezi Disemba mwaka jana.

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka HabNews Tv

Bonyeza HAPA kupakua application yetu na upate habari punde zitufikiapo

Jumapili, 26 Machi 2017

Kiki Za Kisiasa Zamkwamisha Dogo Janja Kuachia Ngoma

Machi 26, 2017 0


Msanii Dogo Janja ‘Janjaro‘ anayetamba na ngoma ya Kidebe amesema hawezi kuachia ngoma yake mpya kama jinsi ambavyo alivyokuwa amepanga kutokana na watanzania wengi kuwa ‘busy’ na masuala ya siasa.
Janjaro amedai anafanya muziki wa biashara hivyo haoni sababu ya kutoa kazi mpya katika kipindi ambacho upepo wa kibiashara haujamnyookea.
“Ukitaka kuuza vitumbua nyako na vikapata soko lazima uuze kipindi cha baridi lakini lazima uwe na chai ya moto, sasa kwa kipindi hiki upepo haujakaa kwenye target yangu maana kila nikiangalia, mara viongozi, huku siasa kwa hiyo nimeona ngoja nitulie nisubiri watanzania wakae sawa” Amesema Janjaro.
Dogo Janja
Hata hivyo Janjaro ameongeza kuwa hana haraka ya kuachia wimbo mpya tofauti na wakongwe wanavyopata ‘presha’ kwa sababu bado anadhani ana miaka mingi katika soko la muziki.
“Mimi bado nina kama miaka 25 ya kuimba muziki na nisipotee kwenye ramani hii, siwezi nikawa na presha kama watu wengine ambao umri umeenda, hata hivyo kwa vile hii ni biashara kila mtu ana target yake ya kuuza biashara yake, ila kwa sababu tayari nimesha ‘shoot’ hadi kichupa sina haraka mambo yatakaa sawa” alimaliza msanii huyo.
Mbali na Janjaro upepo huu wa siasa pia ulimkumba msanii mkongwe Jay Moe ambaye amelazimika kuachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Nisaidie Kushare‘ wiki iliyopita baada ya kushindwa kuutoa tangu mwanzoni mwa mwezi wa pili kwa kuhofia kufunikwa na kiki za siasa.

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka HabNews Tv    

Jumamosi, 31 Desemba 2016

Washindi tuzo za SoundcityMVP2016 King Kiba ndani

Desemba 31, 2016 0

Tuzo za Soundcity  kama ilivyo tuzo nyingine kubwa za vituo vya TV, ni tuzo zinazotolewa na kituo cha Soundcity ambacho maarufu kwa kutoa habari za burudani na muziki masaa 24. Tuzo zilifanyika Lagos NigeriaDecember 29, na Wizkid na Tecno ndio wasanii walioongoza kwa kuondoka na tuzo nyingi.
Alikiba kutoka Tanzania ameiwakilisha BongoFlava baada ya wimbo wake AJE kuchukua tuzo ya video bora ya mwaka. Watanzania wengine waliokuwa wakiwania tuzo hizo ni Vanessa Mdee na Diamond Platnumz.
Nimekusogezea listi ya washindi wa tuzo pamoja na wote waliokuwa wakioania tuzo hizo.
BEST MALE
Diamond Platinumz (TANZANIA)
Emtee (SOUTH AFRICA)
Wizkid (NIGERIA) – WINNER
Falz (NIGERIA)
Olamide (NIGERIA)
Patoranking (NIGERIA)
Phyno (NIGERIA)
BEST FEMALE
Tiwa Savage (NIGERIA)
Victoria Kimani (KENYA)
Yemi Alade (NIGERIA) – WINNER
Vanessa Mdee (TANZANIA)
Cynthia Morgan (NIGERIA)
Ms Vee (GHANA)
Simi (NIGERIA)
BEST HIP HOP
Cassper Nyovest (SOUTH AFRICA) – WINNER
Olamide (NIGERIA)
CDQ (NIGERIA)
Emtee (SOUTH AFRICA)
El (GHANA)
Riky Rick (SOUTH AFRICA)
Stanley Enow (CAMEROON)
Phyno (NIGERIA)
BEST POP
Wizkid (NIGERIA)
Kiss Daniel (NIGERIA) – WINNER
Tekno (NIGERIA)
Yemi Alade (NIGERIA)
Adekunle Gold (NIGERIA)
Timaya (NIGERIA)
Tiwa Savage (NIGERIA)
DIGITAL ARTISTE OF THE YEAR
PSquare (NIGERIA)
Wizkid (NIGERIA)
AKA (SOUTH AFRICA)
Tiwa Savage (NIGERIA)
Davido (NIGERIA)
Cassper Nyovest (SOUTH AFRICA)
Tekno (NIGERIA) – WINNER
BEST COLLABORATION
Mr Eazi Ft Efya – Skintight (NIGERIA / GHANA)
Patoranking Ft Sarkodie – No Kissing (NIGERIA / GHANA)
Eddy Kenzo Ft Niniola – Mbilo Mbilo Remix (UGANDA / NIGERIA)
Emtee Ft Wizkid & AKA – Roll Up (SOUTH AFRICA / NIGERIA)
DJ Maphorisa Ft Wizkid & DJ Buckz – Soweto Baby (SOUTH AFRICA / NIGERIA)
Phyno Ft Olamide – Fada Fada (NIGERIA)
Olamide Ft Wande Coal – Who You Epp (NIGERIA) – WINNER
Harrysong Ft Olamide, KCee – Raggae Blues (NIGERIA)
Masterkraft Ft Flavour & Sarkodie – Finally (NIGERIA / GHANA)
VIDEO OF THE YEAR
Pana – Tekno Directed by Clarence Peters (NIGERIA)
Aje – Alikiba, Directed by Meji (NIGERIA) – WINNER
Babanla – Wizkid, Directed by Sesan (NIGERIA)
One time – AKA, Directed by AKA & Alessio (SOUTH AFRICA)
Sin City – Kiss Daniel, Directed by H2G Films (NIGERIA)
Emergency – D’Banj, Directed by Unlimited L.A (NIGERIA)
Made for you – Banky W, Directed by Banky W (NIGERIA)
Gbagbe Oshi – Davido, Directed by Slash (NIGERIA)
Pray for me – Darey, Directed by MEX (NIGERIA)
BEST GROUP OR DUO
Sauti Sol (KENYA) – WINNER
Mafikizolo (SOUTH AFRICA)
Micasa (SOUTH AFRICA)
Navy Kenzo (TANZANIA)
R2Bees (GHANA)
Toofan (TOGO)
PSquare (NIGERIA)
VVIP (GHANA)
SONG OF THE YEAR
Kwesta ft. Cassper Nyovest – Ngud (SOUTH AFRICA)
Mr Eazi – Hol Up (NIGERIA)
Patoranking ft Sakordie – No Kissing (NIGERIA)
Wizkid – Babanla (NIGERIA)
Tekno – Pana (NIGERIA) – WINNER
Emtee ft Wizkid – Roll Up (SOUTH AFRICA / NIGERIA)
DJ Maphorisa ft Wizkid & DJ Buckz – Soweto Baby (SOUTH AFRICA / NIGERIA)
Olamide ft Wande Coal – Who You Epp (NIGERIA)
D’banj – Emergency (NIGERIA)
BEST NEW ARTISTE
Koker (NIGERIA)
YCee (NIGERIA)
Mr Eazi  (NIGERIA) – WINNER
Emtee (SOUTH AFRICA)
Simi (NIGERIA)
Niniola (NIGERIA)
Tekno (NIGERIA)
Nasty C (SOUTH AFRICA)
VIEWERS CHOICE
Mr Soldier – Falz ft. Simi (NIGERIA) –WINNER
Babanla – Wizkid (NIGERIA)
Osinachi – Humblesmith ft. Davido (NIGERIA)
Pana – Tekno (NIGERIA)
Hollup – Mr Eazi (NIGERIA)
Pick Up – Adekunle Gold (NIGERIA)
Mama – Kiss Daniel
LISTENERS CHOICE
Lagos to Kampala – Runtown ft. Wizkid (NIGERIA)
Babanla – Wizkid (NIGERIA)
Omo Alhaji – YCee (NIGERIA)
Pana – Tekno (NIGERIA) – WINNER
Who You Epp – Olamide ft Wande Coal (NIGERIA)
Oluwa ni – Reekado Banks (NIGERIA)
Pick Up – Adekunle Gold (NIGERIA)
Skintight – Mr Eazi ft Efya  (NIGERIA/GHANA)
AFRICAN ARTISTE OF THE YEAR
Wizkid (NIGERIA) – WINNER
Vanessa Mdee (TANZANIA)
Diamond Platinumz (TANZANIA)
Sarkodie (GHANA)
Yemi Alade (NIGERIA)
Olamide (NIGERIA)
AFRICAN PRODUCER OF THE YEAR
DJ Maphorisa (SOUTH AFRICA) – WINNER
Gospel on the Beat (NIGERIA)
Masterkraft (NIGERIA)
Young John (NIGERIA)
Legendury Beats (NIGERIA)
Sess the problem kid (NIGERIA)
Bonyeza HAPA ku download application yetu

Bonyeza HAPA ku subscribe katika YouTube channel yetu

Ijumaa, 30 Desemba 2016

Rayvan azungumza kuhusu Collabo kati yake na Ali Kiba

Desemba 30, 2016 0

Hakuna asiyejua kama kuna bifu ambalo sio la pole pole kati ya C.E.O wa WCB Wasafi Diamond Platnumz na mtu mzima Alikiba. Bifu ambalo limekaa kibiashara zaidi na hata ushindani katika game.
Waliwahi kusikika Baraka Da Prince ambaye anaonekana kuwa yupo karibu sana na msaniiAlikiba, na hata Abdu Kiba ambaye ni mdogo wa damu wa msanii Alikiba na wakadai kuwa wao hawapo tayari kabisa kufanya collabo na wasanii wa WCB kutokana na kudai aina ya muziki ambao wanafanya ni tofauti na muziki wao.
Sasa leo Perfect255 imemkamata mkali kutoka WCB Wasafi hitmaker wa ngoma ya Natafuta KikiRaymond (@rayvanny) na kupiga nae story imekaa vipi kwa yeye kufanya kazi na msanii ALikiba.
Raymond ametusanua kuwa yeye yuko tayari hata sasa hivi kufanya collabo na Alikiba kwasababu ni msanii ambaye hana tatizo naye na hata wakikutana huwa wanasalimiana vizuri na kusifiana kwa kazi nzuri ambazo wanafanya.
“Mimi Alikiba nikikutana nae huwa napiga nae story, namsalimia, tunacheka, ananiambia mdogo wangu unafanya kazi nzuri. Hatujawahi kukaa sana kwa muda mrefu lakini ikitokea siku naweza kufanya nae,kwasababu end of the day wote tunafanya muziki na muziki ni biashara, mashabiki wanapenda kuona combination za watu tofauti tofauti, ikitokea nafanya nae.”
Bonyeza HAPA kudownload application yetu


Bonyeza HAPA kusubscribe katika YouTube channel yetu

Diamond anyakua tuzo Australia

Desemba 30, 2016 0

Diamond Platnumz amekuwa na mwaka  mzuri sana kwani karibia nyimbo zake zote alizotoa kwa mwaka huu zimeweza kupokelewa vizuri sana mbali tu ya kupokelewa vizuri lakini pia amekwara tuzo kibao kupitia kazi zake.
Mwezi uliopita kituo maarufu cha Radio nchini Australia cha RADIO AFRO AUSTRALIA kiliandaa tuzo za kutafuta nyimbo zilizofanya vizuri kwenye mabara tofauti tofauti na kwenye kipengele cha wasanii waliongiza nyimbo kutoka Bara la Afrika ni Diamond Platnumz kupitia wimbo wake wa Kidogoaliowashirikisha P Square kutoka Nigeria.
Sasa Good News ni kwamba wimbo huo umefanikiwa kuchukua Tuzo ya wimbo bora kwa mwaka 2016 huko Australia. Kupitia mtandao wa Twitter kituo hicho cha Radio kimeandika “#1 radioAFRO Australia Song of the Year 2016 with    

Kwenye kipengele hicho, ‘kidogo’ ya Diamond ilikuwa inashinda na ngoma kama FINAL (Baba Nla)ya WizKid, B.A.D. ya Tiwa Savage, Pana ya Tekno,Soweto Baby ya DJ Maphorisa + DJ Buckz + Wizkid na nyingine nyingi.
Bonyeza HAPA kudownload application yetu
Bonyeza HAPA kusubscribe katika YouTube channel yetu

Jumatano, 28 Desemba 2016

Darasa apata shavu Trace kama nyimbo bora ya Hip Hop

Desemba 28, 2016 0

Kama ni mwaka wa historia ambao unaweza ukaandikwa na rapper Darassa basi huwenda mwaka 2016 ukaandikwa kwa kalamu nyekundu katika kitabu cha kumbukumbu cha rapper huyo.
‘Acha maneno weka muziki’ hiki ni kipande pendwa kinacho wapagawisha wapenzi na mashabiki waDarassa katika nyimbo yake ya ‘Muziki’, na tayari nyimbo hiyo aliyo shirikishwa Ben Pol imeanza kuvuka mipaka ya Tanzania baada ya kutunyoosha takribani miezi kadhaa tangu  kuachiwa kwake.
Kituo cha Trace Africa kutoka Ufaransa kimeucheza mwimbo wa Darassa aliyomshirikisha Ben Pol na kuupa nafasi ya kwanza kama nyimbo bora ya HipHop.
Wasanii wengi wa bongo wameanza kuona matunda ya kazi zao baada ya kuanza kukubaliwa na vituo vikubwa vya kimataifa, ikiwa ni ishara nzuri kuwa muziki wa kibongo bongo sasa umeanza kuota mabawa.
Bonyeza HAPA kudownload application yetu
Bonyeza HAPA ku subscribe katika YouTube channel yetu

Jumanne, 20 Desemba 2016

Joh Makini asema hana shida kwa Lord Eyes kuhama Weusi

Desemba 20, 2016 0
Hatimaye Joh Makini amezungumza kuhusiana na taarifa za Lord Eyez kusainishwa kwenye label ambayo Barakah The Prince ameianzisha. 

Joh amesema pamoja na kuwa Lord Eyez ni mshkaji wake mkubwa, ana uhuru wa kuchukua uamuzi anaodhani una manufaa kwake. 

“Mimi Lord Eyez mbali na muziki ni mshkaji wangu sana, we are family. Hata ninavyoongea na wewe wiki moja nyuma kabla sijaenda South Africa tulikuwa wote usiku huo,” amesema Joh. “Mwisho wa siku unajua naheshimu sana maamuzi ya mtu binafsi na sipendi kuingilia. Kwa mfano siwezi kuongelea uamuzi wa yeye kusainiwa au kutosainiwa na Barakah The Prince sababu that’s him,” ameongeza. 

“Naheshimu kila kitu ambacho yeye anakifanya kwasababu mwisho wa siku kila mtu ana njia yake, ana maisha yake, kila mtu ana maamuzi yake. Unajua huwezi kumuamlia mtu mzima.

Bonyeza HAPA kudownload application yetu

Subscribe katika YouTube channel yetu kwa kubonyeza hapa na uwe unapata matukio na habari kwa njia ya video

Ijumaa, 2 Desemba 2016

Bob Junior Anamchango Mkubwa Sana Kwenye Maisha Ya Diamond

Desemba 02, 2016 0
Diamond hafanyi tena kazi na Bob Junior, lakini hawezi kusahau ukweli kuwa producer huyo wa Sharobaro Records ndiye aliyemfungulia njia ya mafanikio kimuziki. Akizungumza kwenye kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz Alhamis hii kupitia EATV, Diamond alikiri kuwa Bob Junior ana mchango mkubwa kwenye maisha yake.

“Kiukweli Bob Junior ana mchango mkubwa sana katika katika maisha yangu kwasababu ukiangalia nyimbo zangu zote zilizonitoa ni yeye ndiye alikuwa ametengeza,” alisema Diamond.

“Japokuwa hata kipindi ambacho nilikuwa nazitengeneza inawezekana watu walikuwa hawajamuona kama anaweza kuwa producer mzuri sana. Lakini mimi nilikuwa naona mbona huyu natoka naye, nakufa naye mimi yaani huyu natoa nyimbo na inahit,” aliongeza.

“Nakumbuka tulifanya nyimbo kama sita, Nenda Kamwambie, Mbagala, Nitarejea, Binadamu, nyimbo tofauti tofauti. Kila nyimbo alikuwa akinitengenezea akinipa beat nikifika nyumbani naandika vibaya sana. Na mpaka nakumbuka ilifika time niliweka kama chuki fulani kwa wasanii waliopo pale wakaona mbona unampendelea mtu fulani, yeye akasema mimi ni producer, natengeneza beat nikimpa msanii kaandikie kitu kikali, akasema huyu nikimpa analeta beat kali.”

Kwa upande mwingine staa huyo alidai kuwa Mbagala ni moja ya nyimbo zake anazozipenda sana kwakuwa aliuandika kwa ufanisi mkubwa.

Download Application yetu Google Play Store Hapa

Kwa video na habri moto moto bonyeza HAPA na Subscribe kwenye YouTube Channel yetuhannel

Jumanne, 29 Novemba 2016

Diamond Aweka Record Nyimbo Yake Yashika Namba Mbili Uingereza

Novemba 29, 2016 0
Nyimbo mpya ya diamond ft Neyo iitwayo marry you ambayo official release imeshaachiwa United Kingdom (UK) siku chache zilizopita imeendelea kufanya vizuri kwenye vituo mbali mbali.
Katika nyimbo mpya zilizotoka hivi karibuni diamond amekuwa akichuana na Bruno mars na wimbo wake wa Chunky.

Katika nyimbo bora za wiki zilizotoka hivi karibuni marry you imeshika nafasi ya 2 nyuma ya Chunky iliyokamata namba 1 kwenye kituo cha beat london, na kuweka record ya kuwa mtanzania wa kwanza kufikia level hiyo.

Ikumbukwe diamond na Neyo watakuwa na tour ya pamoja mwezi ujao huko UK

Hii ni hatua nyingine muhumu kwa diamond na mziki wake
Ikumbukwe wimbo wa marry you bado haujaachiwa kwa upande wa africa na video bado haijatoka
Japo kuna demo ilivuja

Download application yetu HAPA

Alhamisi, 10 Novemba 2016

Ruby akanusha kusiaini WCB

Novemba 10, 2016 0

Muimbaji wa kike mwenye sauti ya dhahabu kwenye Bongo Fleva, Ruby amefunguka juu ya tetesi zilizosambaa kuwa amesaini kujiunga na lebo ya WCB. 

Ruby amepinga kujiunga na lebo hiyo lakini amedai kuwa anapenda kuwa karibu na Diamond kwa ajili ya kujifunza vitu vingi kutoka kwake. 

“WCB hawana roho mbaya unaenda tu muda wowote kama unajua ni nini kimekupeleka pale, kwani mimi kuonekana WCB ndio nipo WCB? Diamond ni msanii mwenzangu, nikiwa naye najifunza vitu vingi, it doesn’t mean nikiwa naye nimejiunga WCB. Kumbuka pale kuna studio na kuna producer Lizer pale watu tunataka kufanya naye kazi,” amemuambia mtangazaji wa kipindi cha The Playlist cha Times FM, Lil Ommy.

Kwa sasa muimbaji huyo anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Wale Wale’ aliouachia mwezi Septemba mwaka huu.

Bonyeza HAPA kudownload application yetu