Kocha wa Sunderland David Moyes amepigwa marufuku mechi moja na chama cha soka cha England kwa kutumia lugha ya matusi dhidi ya mwamuzi wa mechi amepigwa na faini ya £8,000.
Kisa hicho kilitokea baada ya refa kunyima Sunderland mkwaju wa penalti dakika ya 90 mechi ya Jumatano wiki iliyopita ambapo klabu hiyo ilifungwa 1-0 na Southamptn Kombe la FA.
Baada ya mechi hiyo, Moyes alisema: “Tatizo lilitokea aliponiandama hadi pahala nilipokuwa nimesimama. Nilitumia lugha ya matusi na sikufaa kufanya hivyo.”
Moyes tokea ameteuliwa kuwa meneja wa Sunderland Julai na ameshinda alama mbili pekee kutoka katika mechi 10 za ligi.
Bonyeza HAPA kudownload application yetu na upate habari punde zitufikiapo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni