Uongozi wa klabu ya soka ya Chapecoense ya Brazil ambayo ilipoteza wachezaji wake 19 kwenye ajali ya ndege iliyotokea mwezi Novemba mwaka jana, umepanga kusajili wachezaji wengine 20 kwa ajili ya kuziba nafasi hizo.
Wachezaji wawili walionusurika katika ajali hiyo kati ya watatu akiwemo Neto na Alan Ruschel wanatarajiwa kuwa miongoni mwa wachezaji watakaoichezea timu hiyo, kwa mujibu wa Mkurugenzi wa timu hiyo Rui Costa.
“More than a tribute, we expect Alan and Neto to come back and wear them. Follmann sadly won’t be able to but he will certainly be back here with us in some capacity. The only ones that can wear those jerseys are them,” amesema Costa.
Timu hiyo inatarajiwa kucheza mechi yao ya kwanza kwa msimu huu Januari 26 wakiwa nyumbani dhidi ya Joinville.
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Google Play Store na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka HabNews Tv
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni