.

Ijumaa, 26 Agosti 2016

Ronaldo atwaa tuzo ya mchezaji bora Ulaya


Nahodha wa timu ya taifa ya Ureno anayeichezea klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo usiku wa August 25 aliingia katika historia mpya ya soka lake, hiyo inatokana na kushinda tuzo ya mchezaji bora wa ulaya wa mwaka kwa kuwashinda wapinzani wake Antoine Griezmann wa Atletico Madridi na timu ya taifa ya Ufaransa, pamoja na Gareth Bale.
3794A4FB00000578-3758562-image-a-9_1472143267089
Kutoka kushoto ni Bale, Ronaldo na Griezmann
Ronaldo anafanikiwa kushinda tuzo hiyo baada ya kumaliza msimu wa 2015/2016 kwa mafanikio makubwa ikiwemo kuiwezesha Real Madrid kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa barani Ulaya na kufikisha rekodi ya kutwaa Kombe hilo mara tatu katika historia yake ya soka.
3795021500000578-3758562-image-a-16_1472147165310
Hata hivyo msimu wa 2015/2016 licha ya kuiwezesha Ureno kutwaa taji la Euro 2016 kwa mara ya kwanza katika historia, Ronaldo akiwa na Real Madrid msimu wa 2015/2016 alikuwa kafunga jumla ya goli 51 katika mechi zake 48 alizocheza pamoja na kutoa assist 15, lakini akiwa na rekodi ya kufunga magoli 16 katika mechi 12 za UEFA Champions league.

3794A15300000578-3758562-image-a-5_1472141905887

37949DC600000578-3758562-Ronaldo_signs_autographs_for_fans_before-a-7_1472142976665
37948A0600000578-3758562-image-a-10_1472143292511

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni