.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Ugaidi. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Ugaidi. Onyesha machapisho yote

Jumamosi, 16 Julai 2016

Islamic State wadai kushiriki shambulizi la Nice

Julai 16, 2016 0

Kundi la wapiganaji wa Islamic State limedai kuwa shambulio lililofanywa na mtu aliyewakanyaga watu na lori alikuwa mmoja wa wanachama wake.

Madai hayo yameonekana kwenye mtandao wa kundi hilo unaojulikana kama Amaq.

IS wamekuwa wakitumia mtandao huo kueneza propaganda zao.

Hata hivyo hakuna habari za kuthibitisha kuwa kundi hilo lilihusika moja kwa moja na shambulio hilo.

Tovuti hiyo ya Amaq imekuwa ikieneza taarifa ya IS inayohimiza waislamu kushambulia mtu au watu wanaotoka nchi za muungano wa mataifa yanayoshambulia kundi hilo.

Hata hivyo kuna wanaosema IS imetumia nafasi ya shambulio hilo kujikuza ingawa huenda kamwe hawakuhusika.

Jumatatu, 11 Julai 2016

UN yajadili mapigano Sudan Kusini

Julai 11, 2016 0

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limefanya kikao cha dharura kuzungumzia mapigano yaliyoanza tena nchini Sudan Kusini.

Mamia ya Watu wameuawa tangu kuzuka kwa mapigano hayo Alhamisi iliyopita hadi sasa, katika mji mkuu wa nchi hiyo Juba.
Mapigano hayo ni kati ya vikosi vinavyomuunga mkono Rais wa nchi hiyo Salva Kiir na yale yanayoongozwa na Makamu wa Rais Riek Machar.

Viongozi hao wawili hivi karibuni walisaini makubaliano ya amani ya kumaliza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyodumu kwa miaka miwili.

Awali Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezielezea ghasia hizo zilizoanza tena Sudan kusini, kama zisizo na sababu na hazikubaliki. Amewataka viongozi hao kuyaagiza majeshi yao kujiondoa katika mapigano.

Kwa upande wake Mjumbe wa Umoja wa Mataifa, Sudan kusini Shantal Persaud amesema kambi za pande zote mbili mjini Juba zimeshambuliwa na silaha nzito. Hali inayotishia mamia ya raia kujikuta kuwa wakimbizi.

Aidha amewekea matumaini ya kutekelezwa kwa Makubaliano ya amani yaliyosainiwa mwaka uliopita.

Mshambuliaji Marekani alipanga makubwa

Julai 11, 2016 0

Mkuu wa polisi katika mji wa Dallas amesema wamepata ushahidi kuwa Micah Johnson alifanya majaribio ya kulipuwa vilipuzi.

Kabla ya kuuawa Ijumaa asubuhi, Johnson aliwaambia polisi amekasirishwa na matukio ya hivi karibuni ya mauaji dhidi ya watu weusi yanayofanywa na polisi.
Maafisa watano wa polisi waliuawa katika shambulio hilo.

Jumapili, 10 Julai 2016

Julai 10, 2016 0

Mwanaye aliyekuwa kiongozi wa mtandao wa kigaidi wa al Qaeda Osama bin Laden, ameapa kulipiza kisasi kwa mauaji ya babake.

Katika ujumbe wa sauti uliochapishwa katika mitandao Hamza bin Laden ameapa kulipiza kisasi kwa Marekani kwa kumuua babake 2011 huko Pakistan.

Ujumbe huo wa dakika 21 wenye kichwa "We Are All Osama,", Hamza ambaye inaaminika kuwa alikuwa na babake makomando wa Marekani walipowavamia na kumtwaa ameapa kuendeleza kazi aliyoianza babake.

''Tutaendelea kuwasaka na kuwapiga popote pale mtakapokuwa mumejificha ati nyuma ya pazia za usalama kwa maovu munayoyaendeleza ,Palestina, Afghanistan, Syria, Iraq, Yemen, Somalia na kote kwenye ardhi ya waislamu mnayokalia '' shirika la habari la Reuters linamnukuu.

''na kwa wale wanaodhania kuwa tutakuwa tukilipiza kisasi mauaji ya Osma ole wenu, kwanini sisi tutakuwa tukilinda dinia ya kiislamu'' alisema Hamza.

Osama aliuawa na makomando wa marekani katika maficho yake huko Pakistan mwaka wa 2011.

Hamza ambaye kwa sasa ana umri wa kati ya miaka ishirini hivi alikuwa na babake kabla ya mashambulizi ya kigaidi ya mwaka wa 9/2001 huko Afghanistan kabla ya kukimbilia Pakistan kufuatia mashambulizi makali ya Marekani na washirika wake.

Hamza kulingana na wachanganuzi anatambulishwa na kiongozi wa kidini wa kundi hilo Ayman al-Zawahiri katika ujumbe huo unaolenga kuwavutia vijana ambao kwa sasa wamejiunga kwa wingi na kundi la Islamic state.