.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Uchaguzi. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Uchaguzi. Onyesha machapisho yote

Jumatatu, 31 Oktoba 2016

Sumu ya nyoka dawa ya kumaliza uchungu

Oktoba 31, 2016 0
Joka mwenye sumu kali zaidi duniani huenda akawa jibu la kupatikana dawa ya kupunguza uchungu. Hii ni kwa mujibu ya wanasayansi.
Joka anayejulikana kama 'Blue Coral' ndiye mwenye sumu kali zaidi na hupatikana zaizi Kusini Mashariki mwa Bara Asia. Utafiti mpya uliochapishwa kwenye jarida la afya la Toxin umepata joka huyo huwalenga maadui wake ambao husababisha uchungu kwa binadamu.
Wanasayansi wanasema huenda sumu hii ikatumika kutengeneza dawa ya uchungu. Baadhi ya wanyama ambao sumu yao imetumika kutengeneza dawa ni pamoja na konokono wa baharini na bui bui wa sumu.
Wanasayansi sasa wanataka joka huyu kuhifadhiwa hususan baada ya maeneo mengi anakopatikana kugeuzwa kuwa mashamba ya michikichi. Wanasayansi walifanya utafiti wao katika nchi za China, Singapore na Marekani.
Watafiti wanasema japo kwa mwanadamu nyoka huwa adui, lakini wakati huu huenda akawa suluhu la matatizo mengi ya kiafya.


Bonyeza HAPA kudownload application yetu

Jumatatu, 11 Julai 2016

Matokeo ya Uchaguzi uliofanyika jana Japan

Julai 11, 2016 0

Matokeo ya Uchaguzi uliofanyika jana Japan yanaonesha kuwa serikali ya Muungano inayoongozwa na Waziri mkuu Shinzo Abe, imeshinda

Ushindi huo unampa uwezo kiongozi huyo kuweza kufanyia marekebisho katiba ya nchi hiyo, iwapo ataamua kufaya hivyo.

Amekuwa akionesha dalili za kutaka Japan kujishughulisha zaidi na masuala ya kijeshi, wakati ambapo taifa la Uchina likiendelea kujijenga kuwa taifa lenye nguvu katika eneo hilo.

Hata hivyo, Waziri huyo mkuu wa Japan ameonesha kuwa hata harakisha katika masuala ya kurekebisha katiba. Awali wakati wa kampeni zake alipigia upatu sera ya uchumi.