.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Music. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Music. Onyesha machapisho yote

Jumanne, 11 Julai 2017

21 Savage Akanusha Kununuliwa Gari Na Drake

Julai 11, 2017 0

Rapa 21 Savage amezima stori kuwa alinunuliwa gari ya kifahari aina ya Ferrari na Drake kwaajili ya Birthday yake.
Savage anasema ”Drake alinipa gari aina ya Ferrari nitumie tu wakati nikiwa L.A kwaajili ya Birthday yangu ila lilikuwa la kuazimwa, baadae nilipenda gari kama hio ndio nikanunua Ferrari yake” 
Savage amemsifia Drake kwa kuwa mtu powa kwake kutokana na kumjali na kukumbuka kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa tofauti na wasanii wengine wa rapa.
21 Savage alitoa album mpya July 7 Issa Album.
 

Baraka The Prince Akanusha Kusimamiwa Na Ali Kiba

Julai 11, 2017 0

Msanii Baraka The Prince ambaye yupo chini ya usimamizi wa kampuni ya RockStar4000 amefunguka na kusema kuwa yeye ni msanii aliye chini ya usimamizi wa RockStar4000 na si msanii aliye chini ya Alikiba. 


Baraka The Prince amesema hayo kupitia kipindi cha 5 Selekt na kusema yeye anatambua kuwa Alikiba sasa amekuwa Director wa kampuni hiyo na anaamini anaweza kufanya vizuri lakini yeye hana taarifa zozote juu ya mchongo huo ambao ameupata Alikiba kwenye uongozii wake huo. 

"Mimi sitaki sana kuzungumzia sana juu ya Alikiba kuwa Director wa RockStar4000 kwani kipindi ambacho yeye anaingia mikataba mimi nilikuwa Nairobi na wao walikuwa Afrika Kusini na sijapata nafasi kusikia chochote hivyo kwa sasa bado sijui vizuri hilo jambo, siwezi kulizungumzia japo nafahamu maana naweza kuzungumzia nikazungumza nikasema jambo lisilo la kweli. Ila nimefurahi sababu Alikiba ni kaka yangu na naishi naye vizuri na najua kuwa kazi itakwenda vizuri". Amesema 

Mbali na hilo Baraka The Prince alitoa ufafanuzi kuwa yeye ni msanii anayesimamiwa kazi zake na kampuni ya RockStar4000 na si kusimamiwa na Alikiba kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakidhani au wakihisi hivyo. 

"Mimi ni msanii wa RockStar4000 na si msanii wa Alikiba hilo watu naomba waelewe" alisema Baraka The Prince 

Kwa kumalizia Baraka The Prince alisema watu wengi wanamchukia kutokana na misimamo yake katika kazi yake ya muziki na kudai wasanii wengi wa bongo wamekuwa wakifanya kazi zao kienyeji sana ndiyo maana anapishana nao, kwani yeye anataka kazi ambayo anashiriki iweze kuwekewa mipango na iende katika viwango.

Lil Kim Kuua Bif Kati Ya Remy Ma na Nicki Minaj

Julai 11, 2017 0

Rapa wa kike kutoka Marekani Lil Kim katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa leo anakumbukwa kwa maneno yake ya kujiweka mbali na bifu kubwa linalo fuatiliwa sana na watu wengi nchini Marekani kwa hasa katika muziki wa Rap/Hip Hop kwa upande wa wakina mama.
Related image
Bifu la Nicki Minaj na Remy Ma lilizidi kuwa kubwa baada ya Remy Ma kutwaa tuzo ya BET BEST FEMALE RAPPER  lakini licha ya bifu lao kuwa kubwa Lil Kim alishasikika katika mahojiano na kituo cha Billboard kuhusu Bifu hilo na kusema kuwa hana mpango wa kuungana na Remy Ma kumdiss Nicki Minaj.

Image result for nicki minaj


Lil Kim ambaye alishamdiss NickiMinaj kupitia ngoma ya ‘Black Friday’ aliongeza kuwa hana bifu kabisa na Nicki kwakuwa walishamaliza na kikubwa ambacho anaweza kusema kuhusu marapa hao wa kike ni kuwa shirikisha wote wawili katika album yake mpya.

Sababu Za Wema Sepetu Kutokutokea Katika Video Ya Haitham

Julai 11, 2017 0
Msanii wa Bongo Fleva, Haitham amefafanua sababu ya Wema Sepetu kutoonekana katika video ya ngoma yake mpya ‘Play Boy’ ambayo amemshirikisha mrembo huyo. 



Haitham amesema kulikuwa na mipango ya kufanya video na Wema na script ilikuwa tayari imeshaandikwa ila alipokosekana ilibidi wabadilishe. 

“Na script ambayo tumefanya sasa inayoonekana kwenye video wasichana watatu ilibadilishwa fasta baada ya Wema kutokutokea kwenye video, so script ya mwanzo ambayo Wema alipaswa kuwepo aliandika yeye director na baada ya mabadiliko kutokea akabadilisha scrip,” ameiambia E-News ya EATV. 

Kuhusu athari zilizojitokeza baada ya Wema kutokuwepo kwenye video,  amesema “kwa upande wingine yameathiri kidogo sio sana kwa sababu kuna baadhi ya mashabiki wa Wema walitamani kumuona kwenye video, kwa hiyo ameathiri kidogo kwa wale mashabiki walikuwa wanatamani kumuona,” amesisitiza. 

Play Boy ni ngoma ya pili kwa Wema Sepetu kushirikishwa na msanii wa Bongo Flava baada ya ile ya mwanzo ‘Shoga Yake Mama’ aliyopewa shavu na Snura, lakini hizo zote hakuna hata moja Wema ametokea kwenye video.

Jumamosi, 8 Julai 2017

Wizkid Afanya Maajabu Katika Album Yake Mpya

Julai 08, 2017 0

Msanii kutoka Nigeria Wizkid anategemea kutoa album yake mpya mwezi huu iliyopewa jina Sounds From the Other Side.
CD hii inatoka July 14, kupitia Starboy/RCA/Sony Music International, ikiwa na colabo ya DrakeMajor Lazer, Chris BrownTy Dolla $ignBucie & Trey Songz.
Ty Dolla $ign
Bucie
Chris Brown
Drake
Trey Songz
SOUNDS FROM THE OTHER SIDE TRACKLISTING

1. “Sweet Love”
2. “Come Closer” feat. Drake
3. “Naughty Ride” feat. Major Lazer
4. “African Bad Gyal” feat. Chris Brown
5. “Daddy Yo”
6. “One For Me” feat. Ty Dolla $ign
7. “Picture Perfect”
8. “Nobody”
9. “Sexy”
10. “All For Love” feat. Bucie
11. “Dirty Wine” feat. Ty Dolla $ign
12. “Gbese” feat. Trey Songz

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka HabNews Tv

Bonyeza HAPA kupakua application yetu na upate habari punde zitufikiapo