.

Jumatano, 28 Desemba 2016

Darasa apata shavu Trace kama nyimbo bora ya Hip Hop


Kama ni mwaka wa historia ambao unaweza ukaandikwa na rapper Darassa basi huwenda mwaka 2016 ukaandikwa kwa kalamu nyekundu katika kitabu cha kumbukumbu cha rapper huyo.
‘Acha maneno weka muziki’ hiki ni kipande pendwa kinacho wapagawisha wapenzi na mashabiki waDarassa katika nyimbo yake ya ‘Muziki’, na tayari nyimbo hiyo aliyo shirikishwa Ben Pol imeanza kuvuka mipaka ya Tanzania baada ya kutunyoosha takribani miezi kadhaa tangu  kuachiwa kwake.
Kituo cha Trace Africa kutoka Ufaransa kimeucheza mwimbo wa Darassa aliyomshirikisha Ben Pol na kuupa nafasi ya kwanza kama nyimbo bora ya HipHop.
Wasanii wengi wa bongo wameanza kuona matunda ya kazi zao baada ya kuanza kukubaliwa na vituo vikubwa vya kimataifa, ikiwa ni ishara nzuri kuwa muziki wa kibongo bongo sasa umeanza kuota mabawa.
Bonyeza HAPA kudownload application yetu
Bonyeza HAPA ku subscribe katika YouTube channel yetu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni