Leo November 14, 2016 wananchi kutoka maeneo mengi duniani wameshuhudia tukio la mwezi kushuka chini zaidi ambapo umeonekana kuwa mkubwa kuliko ambavyo huonekana, tukio hili linatokea ikiwa ni tangu ilipotokea mwaka 1948.
Nchi ya Uingereza imekuwa na nafasi kubwa zaidi ya kuuona mwezi huo jioni ya leo Jumatatu, licha ya kuwa umeikaribia dunia zaidi kwa mwendo wa masaa matano na dakika 21 ambapo mwezi huo unakuwa umbali wa kilomita 356,509 kutoka usawa wa Ardhi duniani.
Kwa mujibu wa idara ya hali ya hewa nchi Uingereza Tukio la mwezi kuikaribia dunia litatokea tena tarehe 25 mwezi November 2034.
Bonyeza HAPA kudownload application yetu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni