.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo News. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo News. Onyesha machapisho yote

Jumamosi, 15 Julai 2017

Matokeo Ya Kidato Cha Sita Pamoja Na Ualimu

Julai 15, 2017 0
Matokeo Ya Kidato Cha Sita Pamoja Na Ualimu

Jumanne, 11 Julai 2017

Matumizi Ya Drone Tanzania Kuanza Kufanyika Kwa Vibali Maalum

Julai 11, 2017 0

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imepiga marufuku urushwaji angani wa vifaa vya kieletroniki visivyo na rubani (drones) bila kupata kibali maalum.
Taarifa ya TCAA iliyotolewa kwa vyombo vya habari, imesema kuwa, kwa taasisi au mtu binafsi kufanya majaribio au kurusha drones, ni lazima apate idhini ya Wizara ya Ulinzi na Usalama pamoja na Mamlaka hiyo.
Taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari imefafanua kuwa uendeshaji wa shughuli zote za anga nchini uko chini ya Mamlaka hiyo kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizopo.
Tangazo hilo linakuja wakati ambapo kumekuwa na urushwaji wa drones unaofanywa na watayarishaji wa video za muziki kwa lengo la kupata picha kutokea juu, pamoja na taasisi mbalimbali zinazochukua matukio husika hasa yanapofanyika katika maeneo ya wazi.
Drones zilitumika zaidi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ambapo mikutano ya kampeni za wanasiasa ilikuwa ikipigwa picha za juu kuonesha umati uliohudhuria.

Jumatatu, 3 Julai 2017

Halima Mdee Amkosoa Rais JPM

Julai 03, 2017 0

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Chadema Halima Mdee kwa mwenendo anao kwenda nao Rais Magufuli analipeleka taifa pabaya na kwamba Watanzania wanapswa kumfunga breki kwa kuonesha kutofurahishwa na matendo yake. 

Mdee ameyasema hayo leo Julai 3, wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika makoa makuu ya chama hicho Jijini Dar es salaam, kuhusu kauli ya Marufuku ya mwanafunzi atakayejifungua hatorudi shuleni aliyoitoa Rais Magufuli hivi karibuni. SIKILIZA HAPA CHINI: 



Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka HabNews Tv

Bonyeza HAPA kupakua application yetu na upate habari punde zitufikiapo



Samsung kuingiza simu mpya sokoni baada ya kufeli kwa Galaxy Note 7

Julai 03, 2017 0

Muonekano wa simu mpya za alaxy Note Fan Edition

Baada ya Samsung kulazimika kusitisha utengenezaji wa simu za Galaxy Note 7 kutokana na tatizo lake la kulipuka, kampuni hiyo imeamua kuja na simu mpya ya Galaxy Note Fan Edition.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo imedai, utengenezwaji wa simu hizo umetokana na baadhi ya vitu kutoka katika simu ya Galaxy Note 7 ambayo ilisitishwa kuingia sokoni tangu mwezi septemba mwaka jana kutokana na kuleta madhara kwa baadhi ya watumiaji kutokana na mlipuko kwenye simu hizo.
Taarifa imeendelea kwa kusema simu hizo mpya zitaanza kuuzwa Julai 7 mwaka huu nchini Korea Kusini ambapo ndipo yalipo makao makuu ya kampuni hiyo.

Picha ya simu za Galaxy Note 7 ambazo zilisitishwa kutengenezwa kutokana na kulipuka
Simu za Galaxy Note 7 zilikadiriwa kuuza kiasi cha dola bilioni 5.3 duniani kote ikiwa ni muda mfupi tangu ziingie sokoni lakini baada ya kusitishwa kwa uuzwaji wake inadaiwa kampuni hiyo ilipata hasara ya takribani dola bilioni 10.

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka HabNews Tv

Bonyeza HAPA kupakua application yetu na upate habari punde zitufikiapo

Mwanachuo Aliyeshtakiwa kwa Makosa ya Mtandao Aachiwa Huru

Julai 03, 2017 0

KISUTU: Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemwachilia huru Jovenary Shirima ambaye ni mwanafunzi wa Chuo mjini Arusha aliyekamatwa tangu mwezi Januari mwaka huu akituhumiwa kwa makosa ya mtandao. 

Akizungumza mara baada baada ya kuachiliwa huru, wakili wa Shirima ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu amesema tangu hiyo ufunguliwe upande wa walalamikaji hawakuweza kuendelea kuhudhuria mahakamani jambo lililopelekea kufutwa kwa kesi hiyo. 

“Walalamikaji wameikacha kesi kama walivyokacha walalamikaji wa kesi ya Mbunge wa Arsuha Mjini, Godbless Lema”.

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka HabNews Tv

Bonyeza HAPA kupakua application yetu na upate habari punde zitufikiapo