.

Alhamisi, 15 Septemba 2016

Sababu za Harmonize kuandika nyimbo ya matatizo


Matatizo ni nyimbo ambayo kwa hakika imemgusa kila mmoja katika jamii yetu ya kitanzania. Kwasababu humo ndani Harmonize amezungumzia maisha ambayo wanayapitia vijana wengi wa kitanzania kutokana na ugumu wa maisha na mengineyo.
Harmonize alithibitisha kuwa zaidi ya 70% ya alichokiimba humo ndani kina uhusiano thabiti na maisha yake halisi.
Zipo sababu kedekede zilizomfanya Harmonizekuiandika ngoma hiyo, lakini kitendo cha mkali huyo kushindwa kupenya katika mashindano ya utafutaji vipaji vya kuimba nchini Tanzania (Bongo Star Search) mwaka 2010 ameizungumzia kama sababu kubwa ambayo ilimsukuma kuiandika ngoma hiyo ukiangalia na maisha ambayo alikuwa anaishi kipindi hicho lakini hakuweza kukata tamaa hadi leo ni msanii mkubwa na mwenye mafanikio.
“Sometimes kuna clips zangu ambazo huwa nikiziangalia machozi yananitoka, ukiangalia enzi zile nilikuwa ikifika kipindi cha Fiesta basi mimi saa 8 mchana nakuwa nimesha wasili eneo la tukio ili kuweza kulishuhudia tukio zima. Nimepitia vitu vingi sana ambavyo vimenisukuma kuiandika hii ngoma ya Matatizo na huenda ikawa funzo kwa wenzangu kutokata tamaa na kufanya kazi kwa bidii.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni