Shirika la kukabiliana na dawa za kusisimua misuli duniani WADA limewashtumu wadukuzi kutoka Urusi kwa kutoa faili za siri za matibabu za wanariadha wa Marekani walioshiriki katika michezo ya Olimpiki mjini Rio.
Wanariadha walioathirika ni pamoja na mchezaji wa tenisi Venus na Serena Williams pamoja na mchezaji wa mazoezi ya viungo Simone Biles.
Kundi linalojiita Fancy Bears lilikiri kufanya udukuzi huo kuhusu data ya Wada.Baada ya ufichuzi huo,Bi Biles alisema kuwa amekuwa akitumia dawa za kutuliza mtu kuhangaika.
Kundi hilo la udukuzi lilimshutumu kwa kutumia dawa ya kusisimua misuli,lakini akasema kuwa amekuwa akifuata sheria.
Mshindi huyo wa medali nne katika michezo ya Rio Olimpiki alipata ruhusa ya kutumia dawa hizo zilizopigwa marufuku na Wada ,shirika la wanamichezo wa viungo nchini Marekani lilisema katika taarifa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni