.

Jumamosi, 10 Septemba 2016

Moto waua watu 15 Bangladesh

Watu kumi na watano wameuwawa nchini Bngladesh katika moto mkubwa katika kiwanda kimoja, uliosababishwa na mlipuko wa kifaa cha kuchemsha maji.
Zaidi ya watu 70 wamejeruhiwa viungani mwa mji mkuu Dhaka, na inaarifiwa kwamba huenda idadi ya walioaga ikaongezeka.
Polisi wanasema kwamba zaidi ya watu 100 walikuwa wakifanya kazi katika kiwanda hicho, na kwamba moto huo ulisambaa kwa kasi katika jengo hilo la ghorofa nne.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni