.

Alhamisi, 21 Julai 2016

Desiigner ameachia Cover ya wimbo wake mpya wa “Timmy Tunner”


Baada ya kafanya vizuri na freestyle ya “Timmy Tunner” kwenye XXL’s 2016 Freshman, Rapper Desiigner ameachia cover ya freestyle hiyo ambayo inatarajiwa muda wowote kutoka kama moja ya nyimbo zake.

Timmy Tunner ni moja ya freestyle ambayo iliimbwa na Desiigner kwenye XXL’s 2016 Freshman na kuwafanya mashabiki kwanza kuduwaa kwa kukaa kimya kutokana na uwezo wa Desiigner wa kuchana mistari imekuwaje ameimba “Timmy Tunner”, kadri siku zilivyokuwa zinasogea Desiigner akaamua kuitengenezea ngoma freestyle hiyo na kufanya mashabiki wake kutokea kuikubali.

Kupitia mtandao wake wa Instagram, Desiigner ameweka picha ambayo ndiyo itakuwa cover ya wimbo wake wa Timmy Tunner unaotarajiwa kutoka hivi karibuni, wiki kadhaa nyuma alishawahi kuposti video akiwa studio kuandaa biti la ngoma hiyo ambapo na jana pia aliposti video ikimwonesha anaimba wimbo huo huku akipigiwa kinanda.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni