.

Alhamisi, 21 Julai 2016

Richard Dyle ajibu ishu zinazosema kuwa amefulia


Mshiriki na mshindi wa Big Brother Afrika mwaka 2007, Richard Dyle Bezuidenhout amefunguka juu ya uvumi unaosambaa kuwa amefulia, kwamba pesa alizoshinda kwenye mashindano hayo kumwishia.

Richard Dyle Bezuidenhout ni moja ya watanzania ambao walipata nafasi ya kushiriki na kushinda nafasi ya pili kwenye mashindano ya Big Brother Afrika mwaka 2007 na kufanikiwa kujishindia kitita cha dola laki moja ambacho ni sawa na milioni 200 za kibongo.

Baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu na Kampuni yake ya kutengeneza matangazo na movie, pia kuonekana kwenye baaadhi ya movie ndani ya Industry ya Bongo Movie, Richard ameamua kufunguka juu ya maneno ambayo yanaeleza kuwa amefulia pia na kuzungumzia ujio wa movie yake mpya ambayo imefanyiwa nchini Kanada.

Akiongea na 255, Richard Dyle amefunguka kwa kusema kuwa yeye ni mtu wa privacy sana na amesema kuwa yeye hajafulia kabisa na kuwataka watu ambao wanasema kuwa amefulia waseme ni kitu gani ambacho alikuwa nacho na sasa hivi kikatoka kikapotea.

“Kimyakimya mimi ni mtu privacy sana, sikutaka kupata stress ya watu…..kiukweli hatasahivi niko kimovie kimalengo zaidi kwa ajili ya familia yangu, mi sio ile kuuza sura wala nini, napenda kusikika kitu kile kinachonihusu mimi tu ndio mana sikutangaza,sikutaka mkewangu watoto wangu waanze kuongelewa……………….mi sijafulia washkaji, mimi ni mtu ambaye nina msimamo, ninajipanga na wale ambao wanasema mimi nimefulia nini ambacho walikiona nilikuwanacho kikatoka kikapotea, nini nini……..ambacho mimi nilishawahi kuwatangazia nikaweka hadharani nikajisifia sijui magari majumba kitu gani lishawahi kuwaonyesha nyinyi alafu kesho yake mkaniona mimi sina niko mtaani nazurlula…..labda mseme jamaa kimya, jamaa kapotea hapo nitakubali kweli nilipotea” Alisema Richard.

Richard aliongeza kuwa amerudi na project ya movie mpya inyoitwa “Mchumba sio ATM” ambayo ameshirikiana producer kutoka Kanada.

“Nimerudi na project ya movie moja inaitwa mchumba sio ATM…………tulikuwa tumekuja kuipiga soko ili tuiuze watanzania waijue ipo, ni movie ambayo imepigwa kwa kiwango cha juu, imepigwa kanada na timu ya waswahili,watanzania na wazungu….tumechanganya nchi zaidi ya tano ya Afrika,,,,,,,ni stori ambayo haiko kimapenzi…movie ambayo inaelimisha sana jinsi watu wanavyoishi kanada, wanavyostrugle, watu ambao waliacha vitu vyao huku tanzania,nigeria……ni drama hii itakuwa ni movie yangu ya kumi” Aliongeza Richard.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni