.

Alhamisi, 21 Julai 2016

Nikki wa Pili: Sio tu kusema wasanii wanatutangaza kimataifa, wakati mfumo wa elimu hauitambui Sanaa


Msanii Nikki wa pili kutoka katika kundi la Weusi amefunguka kuwa wasanii wengi nchini wanajifunza sanaa magetoni, mitaani na kwenye mitandao ya kijamii kama You tube na mengine tofauti na fani zingine ambazo elimu yake mtu anaipata akiwa darasani.

Nikki wa Pili aliandika haya kupitia ukurasa wake wa Instgram na kusema inapaswa sanaa nchini ifundishwe darasani kuanzia chekechea mpaka form six kwa kuwa na mitaala katika shule za Umma, tofauti na hali ilivyo sasa ambapo sanaa inaanza kufundishwa chuo.

“Nakumbuka zile takwimu za BASATA zinazo sema Tanzania inakadiriwa kuwa na wasanii milioni 10. Lakini mbona sanaa siioni katika mitaala ya elimu ya umma kuanzia chekechea mpaka form 6. Lakini kuna chuo cha Bagamoyo na Mlimani kuna kitivo cha sanaa sasa hii si ajabu unaanzaje kujifunzia sanaa chuo jamani?

Aliuliza Nikki wa pili kwenye kurasa yake ya Instagram.

Aliongeza kwa kuwaomba viongozi wa serikalini waitazame sanaa kwenye mfumo wa elimu kutokana na kufanya hivyo wasanii watakuwa na maadili kama zilivyokazi zingine.

“Waeshimiwa wote mliopigiwa kampeni na wasanii, hebu jiulizeni hivi hasa wasanii katika mfumo wenu wa elimu, wao wako wapi. siyo tu kusema wasanii wanatutangaza kimataifa, wakati mfumo wenyewe wa elimu wa kitaifa hauitambui sanaa. Ama kusema wasanii hawana maadili, sanaa tunajifunzia magetoni, mitaani, youtube huko kote hamna maadili.

Tungejifunzia darasani huenda kungekuwa na somo la sanaa na maadili. kama tu unavyo jifunza Procurement Ethics…..au maadili ya udaktari” aliandika Nikki wa Pili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni