.

Jumanne, 14 Juni 2016

Mrema kawajibu wapinzani wanaosema Rais Magufuli hazingatii haki za binadamu, katiba


June 14 2016 Mwenyekiti wa chama cha TLP na mbunge wa zamani wa jimbo la vunjoAgustino Mrema amekutana na vyombo vya habari nakuzungumza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuvitaka vyama vya upinzani kutomhukumu Rais Magufuli kwa sababu hana nia ya kuua upinzani kama wanavyodai.
Mbele ya waandishi wa habari Mrema amesema wapinzani ndio waliokubuhu katika kuvunja haki za binadamu, sheria katiba na demokrasia, kama walivyomfanyia na kusababisha kushindwa kwenye uchaguzi wa ubunge jimbo la Vunjo.
Hizi ni sentensi za mrema……>>>‘kwanza  ninachotaka kusema ni kwamba  nataka kuonyesha wapinzani si wazuri kama wanavyotaka Taifa liwaamini si wakweli na wananchi wawe macho sana wasifikiri kila mpinzani ni mkweli wanayoyafanya ni haya lazima tuyafichue  lazima yasemwe waziwazi
>>>’kwahiyo mimi ninachotaka kusema ni kwamba wala sisemi haya kwa sababu ya kutaka kufukua makaburi, nataka watu wajue kwamba  wapinzani vitendo wanavyovifanya sio vya haki na hawamtendei haki Rais, wampe nafasi  aongoze nchi hii wasimsingizie vitu vingi’
>>>Mimi ni mpinzani lakini nitaendelea kuwasema wapinzani ambao hawana deomokrasia, hawazingatii haki za binadamu wala hawazingatii katiba, sheria na ni mafisadi  mimi nitawasema, uwe CCM mimi nitakusema, uwe upinzani nitakusema, wala siogopi wala sitaacha mimi sio CCM, mimi ni mpinzani, mzalendo na mkweli

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni