.

Jumanne, 14 Juni 2016

Usishangae ukisikia Zlatan Ibrahimovic hajajiunga na Man United


Kwa zaidi ya wiki tatu sasa jina la staa wasoka wa kimataifa wa Sweden aliyekuwa anaichezea klabu ya Paris Saint Germain yaUfaransa Zlatan Ibrahimovic, lilikuwa likitajwa kwa kiasi kikubwa kuwa karibu na kujiunga na Man United.
Stori mpya zilizoingia kwenye headlines leo June 14 kuhusu staa huyo ni kuwa mtandao wa 101greatgoals.com umeripoti kunasa mazungumzo ya siri ya staa huyo na FC Bayern Munich ya Ujerumani, mwandishi wa habari za michezo wa kijerumani Raimund Hinko anaripoti Zlatan anashawishiwa ili ajiunge na kocha wake wa zamani Ancelotti.
1,w=816,c=0.sport
Zlatan na Carlo Ancelotti wakati wapo pamoja PSG
Carlo Ancelotti ambaye amewahi kufanya kazi na Zlatan PSG, anadaiwa kutaka kujiunga na FC Bayern lakini anaripotiwa kumuhitaji Zlatan, kwani Robert Lewandowski anaweza kujiunga na Real Madrid hivyo ni vyema akaanza kuandaa mbadala wake, bado haijajulikana na siri inaendelea kubakia kwaZlatan kuwa atajiunga klabu gani?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni