.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Siasa (politics). Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Siasa (politics). Onyesha machapisho yote

Jumatatu, 3 Julai 2017

Halima Mdee Amkosoa Rais JPM

Julai 03, 2017 0

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Chadema Halima Mdee kwa mwenendo anao kwenda nao Rais Magufuli analipeleka taifa pabaya na kwamba Watanzania wanapswa kumfunga breki kwa kuonesha kutofurahishwa na matendo yake. 

Mdee ameyasema hayo leo Julai 3, wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika makoa makuu ya chama hicho Jijini Dar es salaam, kuhusu kauli ya Marufuku ya mwanafunzi atakayejifungua hatorudi shuleni aliyoitoa Rais Magufuli hivi karibuni. SIKILIZA HAPA CHINI: 



Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka HabNews Tv

Bonyeza HAPA kupakua application yetu na upate habari punde zitufikiapo



Alhamisi, 29 Juni 2017

Wakenya Waombwa Wasifanye Mapenzi Siku ya Uchaguzi wa Rais

Juni 29, 2017 0
Mgombea wa chama cha National Super Alliance (NASA) nchini Kenya, Raila Odinga amewaomba wafuasi wake wasifanye mapenzi usiku wa kuamkia siku ya Uchaguzi Mkuu nchini humo. 

Odinga amewataka wafuasi hao kutofanya mapenzi usiku wa tarehe 7/08/2017 ambao ndio utakuwa usiku wa kuamkia siku ya uchaguzi. Alisema kuwa hilo litafanya kila mmoja ajitokeze kupiga kura siku inayofata na kwamba wanaweza kuendelea kufanya mapenzi kwa kusherehekea baada ya kupiga kura. 

“Ukiwa unaenda vitani, kufanya mapenzi ni ishara mbaya,” alisema.

“Baada ya kupiga kura, sasa mnaweza kuenjoy na kusherehekea,” aliuambia umati mkubwa wa wafuasi wake katika mkutano uliofanyika uwanja wa Bukhungu, Kakamega.

Waziri Mkuu huyo mstaafu alisema kuwa Muungano wao wa NASA utahakikisha unahesabu na kutangaza matokeo ya uchaguzi huo. 

“Tutakesha kwenye vituo vyote nchini, tutahesabu kura zetu, tutatangaza tulizopata na kuzilinganisha na zile zitakazotangazwa na Tume ya Uchaguzi,” alisema Odinga.

 Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka HabNews Tv

Bonyeza HAPA kupakua application yetu na upate habari punde zitufikiapo

Jumapili, 30 Aprili 2017

MBUNGE CCM Atuhumiwa Kukwepa Kulipa Kodi ya Milioni 500

Aprili 30, 2017 0


MBUNGE wa Kwimba, Mwanza, Shannif Mansour (CCM), anatuhumiwa kugoma kulipa kodi ya eneo lake la ardhi lenye ukubwa wa hekta 39,000, kiasi cha zaidi ya Sh. 500 milioni tangu mwaka 2010.

Mansour kupitia kampuni yake ya Sineji Tanzania Limited, anatuhumiwa kuigomea serikali kulipa kiasi hicho cha fedha kwa madai yeye hawezi kulipa fedha hizo kwa kuwa anafahamiana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, William Lukuvi.

Eneo hilo la Mansour na kampuni yake inayojihusisha na utengenezaji wa malighafi za ujenzi ikiwemo kusaga kokoto, lililopo kata ya Buhongwa, Nyamagana pia baadhi ya wananchi wanalalamika kulaghaiwa fedha za fidia za maeneo yao.

Tangu kipindi hicho, mbunge huyo alikuwa anadaiwa kiasi cha Sh. 529 milioni na Halmashauri ya jiji la Mwanza na kwamba wakati alipotakiwa kulipa fedha hizo tangu mwaka 2010 alikuwa akigoma kulipa fedha hizo kwa kutumia mwamvuli wa nafasi yake ya ubunge.

Madai ya mbunge huo kuigomea serikali kulipa kodi hiyo, yaliibuliwa jana na Waziri Lukuvi, wakati alipokuwa akizungumza na wakuu kitengo cha idara ya ardhi na wakuu wa vitengo vingine katika Jiji la Mwanza.

Akizungumza katika kikao hicho, Lukuvi amesema kuwa anashangaa kusikia mbunge huyo akigoma kulipa fedha hizo huku watendaji wa halmashauri hiyo wakishindwa kuchukua hatua za haraka ili kada huyo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) alipe kodi ya serikali.

Amesema kuwa katika ulipaji wa kodi wa ardhi watumishi wa idara hiyo wanapaswa kuacha kuangalia kabila wala chama cha mtu kwani waziri hana mamlaka ya kufuta utaratibu wa ulipaji wa kodi lazima ufuatwe.

Hata hivyo, amesema kuwa watumishi hao wanapaswa kuhakikisha ifika Mei 2, mwaka huu wawe wamemchukulia hatua ikiwemo kuangalia utaratibu wa kufuta hatimiliki ya mbunge huyo ili waweze kumuuzia mtu mwingine na kupata mapato.

“Nusu ya lengo lenu la ukusanyaji wa mapato unachangiwa na mtu mmoja (Mansour), haiwezekani mtu mmoja akatae kulipa kiasi hicho cha fedha na nyie mnachelewa kuchukua hatua, utaratibu wa sasa hakuna atakayeshindwa kuchukuliwa hatua kama atashindwa kulipa kodi.

“Eneo lenye ukubwa wa hekta 39,000 sawa na hekari 96, mtu anakataa kulipa kodi, naagiza ikifika, Mei 2, mwaka majibu ya suala hili yawe yamepatikana mara moja, mbunge gani ambaye hataki kulipa kodi,” amesema Lukuvi.

Lukuvi amesema kuwa watendaji wa ardhi jijini hapa, wamekuwa wakishindwa kuwadai kodi wafanyabiashara wakubwa na badala yake wamekuwa wakikusanya kutoka kwa watu wa chini na kuagiza tabia hiyo kukoma.

Afisa Ardhi Mteule Jiji la Mwanza, Silvery Salvatory, amesema kuwa tayari wameisha mchukulia hatua ikiwemo kumfikisha katika baraza la usuruhishi la ardhi mkoani hapa na uamzi wake unatarajiwa kutolewa Mei 5, mwaka huu.

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka HabNews Tv

Bonyeza HAPA kupakua application yetu na upate habari punde zitufikiapo

Ijumaa, 24 Machi 2017

Maneno Ya Zitto Kabwe Baada ya Kumtembelea Nape Nyumbani Kwake

Machi 24, 2017 0

Nimetoka nyumbani Kwa Mbunge wa Mtama ndg Nape Nnauye kumpa Salam zangu za mshikamano na kumtia moyo katika majukumu yake ya kuhudumia watu wa Mtama Lindi na Tanzania Kwa ujumla. 

Amenieleza kuwa anakwenda jimboni kwake ndani ya siku chache zijazo. Nataraji watu wa Lindi, bila kujali itikadi za vyama vyetu vya siasa, watampa mapokezi anayostahili


Alhamisi, 10 Novemba 2016

Msomali wa kwanza kuchaguliwa katika ubunge Marekani

Novemba 10, 2016 0

Ilhan Omar, mwenye umri wa miaka 34, ameweka historia kwa kuwa mbunge wa kwanza mwenye asili ya Kisomalia nchini Marekani.
Mwanamke huyo Muislamu mwenye asili ya Somali na Marekani ndio raia wa kwanza wa Kisomali kuchaguliwa katika wadhfa mkuu kama huo nchini Marekani.
Uchaguzi wake unajiri siku chache tu baada ya rais mteule Donald Trump kushtumu wahamiaji wa Kisomali mjini Minnesota kwa kueneza maoni ya itikadi kali.
Akisherehekea ushindi wake bi Omar amesema kuwa atakuwa sauti ya waliotengwa katika bunge la jimbo hilo.
''Nadhani nimeleta sauti ya akina mama vijana wanaotafuta fursa''.
Redio ya uma katika jimbo hilo ilimnukuu akisema kuwa alitoroka nchini Somalia na familia yake wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe wakati alipokuwa na umri wa miaka minane pekee.
Waliishi nchini Kenya kama wakimbizi kwa takriban miaka minne kabla ya kuelekea Marekani na kuishi katika jimbo lenye Wasomalia wengi la Minnesota.

Bonyeza HAPA kudownload application yetu