Msanii Linex Mjeda leo alitoa nafasi kwa mashabiki wake kumuuliza maswali na yeye kutoa majibu ya maswali hayo kupitia Account yake ya Twitter, ambapo watu waliweza kuuliza maswali na yeye kutoa majibu ya maswali hayo.
Moja ya shabiki yake alimuuliza kati ya Jokate Mwegelo na msanii wa Kenya, Avril ni yupi anaweza kumchagua ndipo star huyo ambaye ametamba na ngoma kibao kali aliposema kuwa hajawahi kuwaza jambo hilo, na sababu ya kutokuwaza jambo hilo ni kutokana na ukweli kwamba warembo hao ni wazuri mno kiasi kwamba anahisi yeye si chaguo sahihi kwa watu hao kuotokana na uzuri wao.
“Sijawahi kuwawazia kabisa labda kwa sababu niwazuri sana that’s why naona mimi siyo type yao’ aliandika Linex Mjeda.
Lakini mbali na hilo Linex alisema kuwa yeye anafanya muziki kutokana na hisia hivyo asipokuwa na hisi na muziki hawezi kufanya kazi yoyote ile hata wiki nzima au hata zaidi mpaka pale atakapopata hisia za kufanya kazi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni