.

Alhamisi, 23 Juni 2016

Je unatamani kumuoa Linah? Fahamu hili


Ikiwa wewe ni miongoni mwa washkaji ambao umepanga kumchumbia mwanadada Linah, Taarifa ikufukie kwamba hana shida na kuolewa anachowaza ni kuwa na mtoto kwa sasa.

Akiongea na 255 Linah amezungumza kuwa ameona matukio mengi sana ambayo yanatokea kwenye ndoa ndiyo yanayomfanya kuchanganyikiwa kufikiria kuingia kwenye maswala ya Ndoa na kuwaza kuzaa mtoto

“Sanasana nafikiria sana mtoto kuzaa, Naona matukio mengi sana ambayo yanatokea kwenye ndoa, nikikaa kufikiria maswala ya Ndoa nahisi kuchanganyikiwa, ila mwisho wa siku mi naona ni mdada nakuwa mkubwa almost miaka 26, mama yangu pia anahitaji mjukuu na mimi nafikiria sana kufanya hivyo vitu, najua pia mama yangu sometimes anafikiria maswala ya ndoa, heshima ya mwanamke ni ndoa sawa” Alisema Linah
Kuhusu kwamba labda watu wa kumwoa hawapo, Linah amesema watu wapo wakumwoa ila sio waoaji wengi ni wadanganyaji kwa ndoa

“Sio kwamba wanaotaka kunioa hawapo, wapo lakini naona kama mh, yani mtu anakudanganya kwa ndoa halafu anakuchumbia alafu mwisho wa siku ndiyo basi, kwahiyo zile stori alichumbiwa na flani, hata ndoa haikufika Dahh..zile stori zinaniuma sana…Bora ionakane kwamba alizaa basi, ila mi nikifika miaka 30 yes, yani hapo nipotayari kuolewa kabisa ni ndoa kama mke, kuwa na mtoto hata Kesho sema wakuzaa nae jamani, naangalia Baba mwenye uwezo wa kulea mtoto”Aliongeza Linah

Mwanadada Linah alishawahi kupiga stori na 255 kuhusu rapper Darassa, miongoni mwa watu ambao wanasifa za kila kitu ambazo Linah anazitaka kwa mwanaume ndizo alizonazo Darasa na anatamni kama angekuwa amezaa nae coz anasifa zote za kuitwa Baba.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni