.

Alhamisi, 23 Juni 2016

Rich Mavoko: Kama WCB wangekuja na gear ya kunipa gari au nyumba basi ningewachomolea kujiunga nao


Imekuwa kawaida siku hizi kwa Mameneja wa bongo kuwazawadia wasanii wao magari au nyumba.

Hili limekuwa ni jambo la kawaida ambapo hivi karibuni june 11 mwanamuziki Msami aliweza kuzawadiwa mkoko aina ya Toyota Ipsum wenye thamani shilingi milioni 15 na meneja wake.

Jana june 22 kupitia 255 ya clouds fm, Mavoko ameweza kufunguka haya “kikubwa mimi nilichoangalia ni biashara yangu kufika sehemu fulani, kwa sababu unajua tunapofanya kazi na watu wengi kuna vitu vingi unakua unapata tofauti na unapofanya kazi peke yako, napia time zikawa zimekaa sawa kabisa yani kwa mwaka mmoja tumefanya hichi na hichi, kuna vitu ambavyo vinabadilika katika biashara kama wangekuja kwa njia ambayo watanipa gari au nyumba kwa kweli ingekuwa ngumu na sio kwamba wangekuja kwasababu mimi na wao hakuna mtu aliyemtafuta mwenzake so nimaongezi tu yamefanya tumekutana lakini pia wameonesha wana nia yakufanya”.

Mavoko aliendelea “tufanye biashara, tusifanye hii iwe sehemu ya mtu kumsindikiza mwenzake kwenye utajiri..hapana.. sisemi mtu asichukue ila msanii unapoambiwa utapewa gari na nyumba basi ukapapatika kwenda kusign mkataba, jiulize anaekupa anakuwa anania gani na hivyo vitu kwa hiyo we unashindwa kuvipigania mpaka ukavipata hivyo vitu, mi gari ninalo na kama nyumba, nyumba ninayo au sio na hata kama sikai mimi anakaa wanakaa ndugu zangu, mama yangu lakini sasa nyumba ninayo, tuangalie biashara yetu inafika wapi au biashara yako inafika wapi kwa miaka fulani. inabidi uwe unaishi kwa mipango pia maana inasaidia hasa kwa sisi vijana kuishi kwa mipango, kwamba mwaka huu na mwaka uliyoisha nimeishi tofauti yani nimetumia kiasi gani au nimepoteza kiasi gani, au kimeingia kiasi gani au nimebadilika nini”.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni