.

Jumanne, 14 Juni 2016

BABU TALE KAKUBALI KUYAJIBU MASWALI BAADA YA KUPIGA PICHA NA ALIKIBA


Taasisi ya GSM foundation inayofanya kazi ya upasuaji wa vichwa vikubwa na migongo wazi, wiki iliyopita iliandaa hafla ya futari ambayo ilihudhuriwa na wasanii mbalimbali pamoja na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.


Hafla hiyo ambayo lengo lilikuwa kukutanisha wasanii mbalimbali kwa kuungana pamoja ili kuwa kama chachu ya elimu ya afya katika jamii na Tanzania kwa ujumla.

Moja kati ya picha zilizopigwa kwenye hafla hiyo ambazo zimeleta gumzo kwenye mitandao ni ile ya Meneja wa Diamond Babu tale kuwa karibu na alikiba wakiwa na furaha, ilitengeneza maswali mengi kwa mashabiki wa muziki Bongo fleva.

Akiongea na 255, Babu tale amesema kuwa inabidi ifikie wakati wa tanzania wabadilike kwamba hawawezi kutengeneza dhama ya kwamba WCB hawawezi kupiga picha na Alikiba, hizo ni vita za kibiashara tu.

“Huwezi kutengeneza dhama kwamba sisi tuna matatizo, hatuwezi kupiga picha kukaa pamoja hatujafikia hatua hiyo, tunabishana kimuziki tu, haimanishi kuwa diamond na Kiba wanavita, watu hawajui kuwa kuna picha ambazo sisi tunazo za kiba na Diamond wanaongea na wako studio pamoja……ile ilikuwa ni picha ya kawaida kwasababu alianza kuitwa Mwana fa akafuata Ali, then nikafuata mimi na Sallam, kama nisingekuwa sitaki kupiga ningekimbilia upande wa Sallam” Alisema Babu tale.

“Kwasababu kabla ya kufuturu tulikaa safu moja kwenye kuswali na wala hatukuwa na masuala yeyote ya muziki”aliongeza Babu tale.

Hata hivyo mashabiki wa wasanii hao hawakuishia hapo kuhusu picha hiyo na kuanza kusema kuwa Diamond platnumz aliamua kuuchuna baada ya kusikia Ali kiba naye ni miongoni mwa wa wasanii walioalikwa katika hafla hiyo.

Tale nalo alilizungumzia kupitia 255 na kusema kuwa Diamond hakuwepo siku ya mwaliko huo na vilevile aliwatowa hofu kuhusu bifu la Diamond na Ali kiba.

“Diamond hakuwepo coz alienda kufanya tangazo siku aliyoalikwa ndio maana hakutokea..Alafu niwatowe hofu kuwa mimi Babu tale sina tatizo na Ali kiba coz nafanya Biashara…wala Nasibu naye hana bifu na kiba hata mara moja ,hizo ni vita tu za kibiashara ambazo zinakuza soko la muziki nchini tofauti na ilivyokuwa zamani”Alimalizia Babu tale.

Kuhusu swala la Uongozi wa WCB kupiga picha na Ali kiba lishaonekana mara kibao, miongoni mwa picha hizo ni ile wakatai Diamond platnumz anatambulisha ujio wa ngoma yake “kama utanipenda” ambayo Sallam aliposti picha katika kurasa ya instagram akiwa na Ali kiba na kuweka
#mara umeneja na diamond platnumz na WCB umefika kikomo na kuamua kwenda kwa Kiba

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni