Meneja huyo wa Rapa Young Killer kutoka Mwanza amesema kuna changamoto kadhaa zilizotokea na kusababisha kuchelewa kwa video ya ngoma ya Msodoki Mtafutaji lakini kila kitu kimeshakuwa sawa na mwishoni mwa wiki hii wataiachia rasmi.
Calisah pia ameelezea mipango waliyonayo kama management na msanii husika ikiwemo kuachia ngoma mpya hivi karibuni .
Amesema ngoma hiyo itakuwa kama zawadi tu kwa mashabiki wa Young Killer lakini anaamini itafanya poa sana kutokana na ukali wake.
Mbali na hilo Calisah ni video modal pia na alishaonekana kwenye video kadhaa ikiwemo Kumekucha ya Young Killer akimshirikisha Mr Blue lakini umaarufu wake umekuwa zaidi katika story za hivi karibuni kutoka kimapenzi na Wema Sepetu
Bonyeza HAPA kudownload application yetu na upate habari punde zitufikiapo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni