.

Jumanne, 1 Novemba 2016

Ally Kiba aja na lebo yake Jokate, Abdu Kiba, Abby Skils ndani


Imekuwa ni kama fashion sasa kwa wasanii wa Bongo Fleva kwa kila mmoja kutaka kuwa na lebo yake, ukiachilia mbali wale ambao walikwisha tangulia kwenye mambo hayo na lebo zao zikafanya poa.
Alikiba ameichanaPerfect255 kuwa kuhusu suala la Lebo yeye ameshawahi kuwa nayo kitambo, na kuna wasanii ambao alikuwa akiwasimamia lakini kwa muda fulani alikuwa amepumzika kidogo juu ya jambo hilo.
King Kiba ameitobolea siri Perfect255 kuwa yuko katika maandalizi ya kurudi rasmi katika suala hilo la kusimamia wasanii (Kuanzisha Lebo) na tayari kuna wasanii ambao amekwisha fanya nao mazungumzo na watakuwepo chini ya lebo hiyo.
“Me record lebo ninayo muda mrefu, lakini sikuifanya matangazo, lakini kuna wasanii ambao nilikuwa nawamiliki nikapumzika, sasa hivi narudi tena najipanga upya kama unavyomuona Abby Skills anafanya kazi vizuri na bado ataendelea kufanya kazi zingine, Abdu Kiba pia ametoa ngoma hivi karibuni lakini haijafanya vizuri lakini ngoma ijayo itakuwa ni ya mimi na yeye. Pia kuna msanii mwingine ambaye watu hawajawahi kumsikia, pia kuna wakina Jokate, kina Dalila na wengine kibao tu ambao wapo chini ya Lebo yangu.”

Bonyeza HAPA kudownlod application yetu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni