.

Ijumaa, 7 Oktoba 2016

Usichokijua kuhusu All The Way Up version ya Diamond


Ilikuwa tumsikie Diamond kwenye Remix Hit ya ‘All the way up’ version ya Afrika.
Diamond amesema Remix hiyo ilikuwa iwashirikishe wasanii kutoa Afrika Mashariki, Magharibi na Afrika kusini ikiwemo Yeye mwenyewe, Wizkid na msanii mwingine wa Afrika kusini.
“Hii nyimbo kwanza ilitumwa kutoka America, walikuwa wanataka African version yani remix ya Afrika, ilitakiwa niwepo Mimi, Wizkid na kuna mtu yupo South Africa sijui nani jina lake, so walichagua East Africa, West Africa na South Africa ” Diamond alifunguka kwenye kipindi cha Daladala Beats cha Magic Fm.
Diamond amesema aliamua kuachia verse yake baada ya kuona wanachelewesha Remix hiyo.
“So kila mtu akafanya verse yake, nafikiri mimi nilikuwa wa kwanza kufanya kwasababu nilikuwa nimeipania sana, so baada ya kufanya ndio ile version ya kwanza, nikaona wanachelewesha, nikaona mbona hawaachii, nikatia verse yangu Instagram, naona watu fresh nikakaa basi nikaongea na uongozi wangu nikawaambia sikiliza, naona kama jamaa wanachelewa mimi wanipe permission niifanyie verse mbili zote alafu nitoe version ninayoijua mimi, so wakazungumza nikaandika verse ya pili pia

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni