.

Ijumaa, 7 Oktoba 2016

Baraka kuja na lebo yake ya BANA


Muimbaji wa ‘Nisamehe’ Baraka amezungumzia mpango wake wa kufungua label yake ‘BANA’ itajayosimamia wasanii, kutengeneza nguo na chakula.
“BANA ni Baraka and Najma, ni kampuni itakayokuwa na vitu vingi vingi,” Baraka alifunguka kwenye Enewz “Kutakuwa na recording lebel, itakuwa na masuala ya mavazi, yani tunataka kutengeneza nguo ambazo zina lebel yetu, na pia kutakuwa na masuala ya chakula humo humo, so ina mambo mengi mengi tofauti”
Baraka ambaye yupo chini ya Rock Star 400 amesema hata hivyo yeye hatokuwa mstari wa mbele sana katika kusimamia wasanii ambao watakuwa chini ya label yake,
“Ujue kusimamia wasanii siyo mimi ndo nitakuwa nipo front sana, kutakuwa na mameneja, kila msanii atakuwa na meneja wake, ina maana mimi sitakuwa nahusika moja kwa moja na wasanii, ila nitakuwa kwenye management”. Baraka alielezea.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni