.

Jumatatu, 10 Oktoba 2016

Snura afunguka kuhusu Chura


Duh! kwa kukomaa huko! Hivi ndivyo unavyoweza kusema mara baada ya kibao cha Chura, chake msanii Snura Mushi kuruhusiwa kuchezwa baada ya kuwa kifungoni kwa miezi kadhaa sasa.
Serikali kupitia Baraza la sanaa la Taifa (Basata), chini ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ilifungia wimbo huo Mei, 4, mwaka huu kwa maelezo kwamba maudhui yake hayana maadili kwa jamii yetu ya kibongo.
Katika maelezo ya Basata, Snura alitakiwa kutoshiriki kwenye shoo yoyote mpaka pale atakaporekebisha video ya wimbo huo na kuruhusiwa kuendelea na shughuli zake za muziki.
Lakini juzi, Jumatano Snura alisema kuwa wimbo wake huo umeshafunguliwa na serikali baada ya kurekodi upya video ya wimbo huo ambayo sasa ina maadili ya Kitanzania.
Kwa kawaida wasanii wengi ambao nyimbo zao hufungiwa, huachana nazo na kuendelea na nyingine, lakini kwa Snura imekuwa tofauti baada ya kuamua kukomaa hadi alipotimiza masharti yote na kuruhusiwa kuendelea na Chura wake.
Je, nini kimemfanya ang’ang’anie kwa nguvu zake zote kurejesha wimbo huo. Kupitia Swaggaz Snura aliweza kufunguka:
“Nimekubaliana na maelekezo ya serikali na nimebadili video ya wimbo wangu wa Chura na sasa umeruhusiwa rasmi. Lakini najua watu wengi watakuwa wanajiuliza kwa nini nimeng’ang’ania huo wimbo? Kwanini nisingeendelea na nyingine nikaupotezea Ukweli ni kwamba, Chura ndiyo kama utambulisho wangu.
“Bila Chura hakuna Snura, ndiyo maana nikaamua kutumia nguvu zangu zote kuurudisha. Kila mtu anafahamu kuwa Chura ndiyo wimbo wa kwanza wa Singeli kutamba kabla hata wanamuziki wengine hawajasikika.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni