Weekend iliyopita akili na mawazo yote ya wapenda burudani Africa Mashariki yalikuwa katika mji wa raha Mombasa nchini Kenya.
Kutokana na Tamasha kubwa la muziki ambalo lilimdondosha staa wa muziki kutoka nchini Marekani Chris Brown kufanyika mjini humo. Tamasha ambalo lilifahamika kama Mombasa Rocks Music Festival.
Tamasha hilo lilikumbwa na drama za hapa na pale ukizingatia Chris Brown kuvunja simu ya Shabiki kisa kuomba selfie na mengineyo.
Lakini kibongobongo kilicho kiki zaidi ni kile kitendo cha msanii kutoka Tanzania Alikiba kuzimiwa mic na kutakiwa kushuka kwenye steji kabla ya muda wake kuisha ili apande Chris Brown, na baadae mkali huyo kutoka Marekani alivyomaliza ndio King Kiba kurudishwa tena stejini kuendelea na show.
Wengi hawakupendezwa na kitendo hicho akiwemo muhusika mwenyewe Alikiba. Na baadae alipofanyiwa interview, Alikiba alidai kutilia mashaka uwepo wa Sallam SK ambaye ni meneja wa msanii Diamond Platnumz backstage, na kudai kuwa hakuona sababu iliyomleta Sallam backstage wakati yeye anafanya show.
“Kuna vitu ambavyo sijavielewa ambavyo vilikuwepo pale, na pia sijafurahishwa navyo. Nilimuona meneja wake Diamond alikuwepo pale, na sikuelewa alifuata nini backstage wakati mi naperform, yeye anahusika kama nani? haileti picha nzuri.”
Hayo ni baadhi tu ya maneno kati ya mengi ambayo aliyazungumza Alikiba baada ya kutokea kilicho tokea kwenye show hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni