.

Jumatano, 19 Oktoba 2016

Disney yaitolea nje Twitter

unnamed
Kampuni tajiri ya Walt Disney, ilisita kununua mtandao wa kijamii wa Twitter kutokana na kasumba ya unyanyasaji inayofanywa na watumiaji wake ambayo ingechafua heshima yake, kwa mujibu wa ripoti ya Bloomberg.


Disney ilikuwa moja ya makampuni ambayo ilikuwa imetajwa kuwa kwenye mazungumzo ya kutaka kuununua mtandao huo unaotapatapa kifedha.
Tweets za matusi na kejeli zimekuwa maarufu kwenye mtandao huo. Mfano pindi Robin Williams amefariki, baadhi ya watumiaji wa Twitter walimshambulia binti yake hali iliyomfanya aifute app hiyo kwenye simu yake.
Mtandao huo umeshindwa kuhimili ukuaji wa mitandao mingine kama Facebook, Instagram na Snapchat.

Download application yetu na upate habari punde zinapotufikia HAPA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni