.

Jumatano, 19 Oktoba 2016

Barak Da Prince eti akana kumfahamu Alawi Junior

Story iliyokiki zaidi siku ya jana ni kuhusu ile nyumba ambayo siku chache zilizopita msaniiBaraka Da Prince alijitapa kuwa amejenga yeye na mpenzi wake Naj.
Ni baada ya msanii Alawi Junior ambaye ni mzazi mwenzake na dada yake Naj (Lady Naa) kupost katika ukurasa wake wa instagram nyumba hiyo na kuandika caption ya kumpongeza mama mzazi waNaj kwa kununua nyumba.
Kitendo ambacho kilizua maswali mengi ya sintofahamu na wengi kujiuliza kuwa huenda Alawiakawa na bifu na Baraka Da Prince au ni kweli ile nyumba sio ya Baraka bali aliamua kujitapa tu ili aonekane anacho kumbe hana.
Soudy Brown ameamua kukata utepe wa sakata hilo, ni baada ya kuwapigia simu wote wawili naAlawi Junior akafunguka kila kitu kuhusiana na nyumba hiyo. Anadai ina thamani zaidi ya million 200 na ilinunuliwa na mama mzazi wa Naj, na yeye alihusika katika ununuzi wa nyumba hiyo.
Baraka Da Prince alipopigiwa simu alidai kuwa hamjui kabisa mtu anaeitwa Alawi Junior na wala hataki kumzungumzia kwasababu anahisi atampa faida bure.

Download application yetu HAPA na upate habari punde zinapotufikia

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni