Bado headlines za mfanyabiashara na bilionea namba moja Afrika mpango wake wa kutaka kuinunua Arsenal haujafa katika kichwa chake na bado ana imani ipo siku atakamilisha mpango huo Aliko Dangote, bilionea huyo tayari ameweka wazi tena katika interview zake kuwa lengo lake bado lipo palepale.
Aliko Dangote ambaye ni bilione namba moja Afrika ni miongoni mwa raia wa kigeni waliowekeza Tanzania, Dangote ndio mmiliki wa kiwanda cha Cement kilichopo Mtwara, kwa mara ya kwanza Dangote alitaka kuinunua Arsenal mwaka 2010 lakini lengo lake hilo halikutimia.
Bilionea huyo ambaye ambaye anatajwa kuwa na utajiri wa zaidi ya dola bilioni 10.9 unaotokana na biashara zake mbalimbali zikiwemo za Cement na bidhaa mbalimbali amenukuliwa kituo cha TV cha New York bado hajaonesha kukata tamaa na mpango wake.
“Bado na matumaini ipo siku kwa bei sahihi nitainunua Arsenal, naweza kuinunua ipo siku bali sio kwa pesa kidogo ila ni kwa bei ambayo wamiliki hawatotaka kuikataa, najua mipango yangu labda katika kipindi cha miaka mitatu au minne baadae”
Asilimia 67 ya hisa za Arsenal inamilikiwa na bilionea wa kimarekani Stan Kroenke na mabilionea wawili wengine Alisher Usmanovna Farhad Moshiri wao wanamiki asilimia 30 ya hisa za Arsenal.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni