.

Alhamisi, 22 Septemba 2016

Aliyoyasema Davido baada yakuto kuchaguliwa kuwania tuzo MTV MAMA


Nomination ya Tuzo za MTV MAMA imetoka na kilichowaacha watu wengi ni mshindi wa tuzo ya Kipengele cha ‘Best Male’ kwa miaka miwili mfululizo kukosa nomination mwaka huu.

Davido ambaye hajaachia wimbo mpya tangu mwaka umeanza suala la kukosa Nomination kwenye tuzo hizo halijamshitua yeye mwenye, Davido amedai ni haki kabisa kukosa tuzo hiyo huku akijigamba kwa tuzo tuzo tatu za MAMA alizoshinda ndani ya miaka miwili.
“I really shouldn’t be nominated this year For what?? I got three MAMAS in two years I’m good ! Still gonna be a great show! BUT NEXT YEAR” Davido amemjibu mmoja wa shabiki yake aliyehoji kuhusu tuzo hizo.
Hata hivyo hii ni awamu ya kwanza ya Nomination na Davido ameambulia kwenye Best Collabo kupitia wimbo wa rapper wa Afrika Kusini Nasty C ‘Juice Back
Remix’ ambao pia Cassper Nyovest ameshirikishwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni