.

Jumamosi, 16 Julai 2016

Usiyo yajua kuhusu The Amazing ya Izzo Bizness na Abella Music


Yapata wiki mbili sasa toka hit maker wa single ya “Shem Lake ” anaye represent Mbeya City Izzo Bizness alizindue kundi lake jipya la The Amazing ambalo linaundwa na watu wawili ambao ni yeye na mwanadada Abella Kutoka nchini Marekani.

Kumekuwa na sintofahamu kwa mashabiki wa mwanahiphop huyo na wapenzi wa muziki wa Bongo fleva pia juu ya Izzo Bizness na mwanadada huyo walikutana vipi hadi kufikia kuunda kundi hilo la The Amazing.

Izzo Bizness amefunguka baada ya kusogezewa kipaza cha 255 na haya hapa ndio yalikuwa majibu yake.
“Mwanzo tulianza kuwasiliana kupitia mitandao ya kijamii, kikubwa ambacho alikuwa ananieleza ni kwamba yeye ni fan wangu mkubwa na anafuatilia muziki wangu na ana wish siku moja kuja kufanya kazi na mimi.

Ilianza kama maongezi ya kolabo, mwisho wa siku nikapitia kazi zake ambazo alikuwa ananitumia link nikagundua kuwa ana talent, kuna ngoma tulirekodi tuka mtumia kipindi bado yuko nje tukamwambia afanye chorus. Mwisho wa siku akafanya na akatutumia ngoma ikawa imesimama. Kwakuwa alikuwa na safari ya kuja Tanzania tukaanza kufanya mipango ya yeye akija huku ndio tufanye Project iliyo kamilika tukiwa wote studio kwa sababu huwa inakuwa vizuri kama mnafanya kitu wote mkiwa studio.

Alivyo kuja Tanzania tukafanya kazi baada ya kazi tukaona kuwa chemistry ipo na baada ya hapo tukakaa na kuongea kuwa tunaweza kutengeneza jitu lakini mwisho wa siku kila mtu anaweza kufanya projects zake kama wasanii binafsi nje ya the Amazing.” Alifunguka hayo Izzo Bizness.

Izzo aliongeza kuwa The Amazing haitoishia kwa wao wawili tu! Kama ikitokea kufanya usajili watafanya ili kukuza kundi na kulifikisha mbali pia.

Kama unavyo mjua Izzo Bizness ni mtu wa fashion, The Amazing pia hakuiacha nyuma katika swala hilo na ameweka wazi kuwa kundi hilo litajihusisha ku brand nguo, viatu na vinginevyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni