.

Jumamosi, 16 Julai 2016

Baada ya kuimbwa kwenye ngoma ya “Kaa tayari”, Babu tale amefunguka haya kwa Roma


Rapper Roma Mkatoliki kuachia video na audio ya wimbo wake mpya wa “Kaa tayari”, Sasa kama umeisikiliza vizuri ngoma hiyo, kuna mistari Roma amemdisi Babu tale iliyosema “Boss kamganda Dangote kaisahau TipTop”, Baada ya kusikia laini hiyo, Babu tale amefunguka haya.

Akiongea na 255, Babu tale amefunguka kuwa Roma ni mtu ambaye huwa anategemea taarifa ya Habari ndiyo aandike wimbo wake kwahiyo yeye kama Babu tale anasema inabidi Roma apewe sapoti kwasababu zisipo patikana atapotea kwenye game.

“Roma ni mtu ambaye anaimba mashairi kama anasubiria taarifa ya habari itoke,ni mtu ambaye anasubiria radio zitangaze taarifa ya habari, media ndio aandike mashairi………kwahiyo usipomsapoti Roma maanake umtamkii Roma maisha yake kua mema kwenye mziki, unatamani Roma apotee sio nzuri unapata dhambi, kwahiyo sasa hivi ameamua kuja huku sasa, huku sio kwake ni kwa Nay wa mitego, kwa kasi hii ya magufuli itakuwa nguma sana……kwasababu Roma alikuwa anategemea taarifa ya habari ndio aandike nyimbo……….” Alisema Babu tale.

Tukirudi upande wa pili wa Saidi Fella baada ya kuongea na Planet Bongo, amezungumza kuwa Roma ni mtu mzima na anavyoviimba vyote vinasemwa mtaani, lakini pia Saidi Fella alishamsisitizia Babu tale kwamba wafanye yote ila Babu tale asiisahahu TipTop Connection na yeye Fella asiisahau TMK.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni