.

Jumanne, 19 Julai 2016

Usicho kijua kuhusu Kolabo ya Davido na Joh Makini


Kama uliwahi kuisikia hii ya Rapper wa kitanzania Joh Makini kuja na kolabo ya kimataifa na hit maker wa single ya Fans Me aliyo mshirikisha Meek Mill kutoka marekani, Davido hii ni exclusive nakupa kwamba nyimbo hiyo iko mbioni kutoka hivi karibuni.

Akihojiwa katika The Base ya ITV rapper
Joh Makini amelithibitisha hilo na akatuhabarisha kuwa kitu kizuri katika nyimbo hiyo ni kwamba Davido ameimba kiswahili kwenye chorus nzima ya nyimbo hiyo.

Ni jambo zuri na lenye faida kwetu na kwake pia ambapo kwa upande wake itamuongezea mashabiki na watu wanaosikiliza muziki wake kwa ukanda huu unaozungumza lugha ya kiswahili.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni