.

Jumanne, 19 Julai 2016

Haikuwa rahisi SIMBA kutokea kwenye video ya “Kidogo” : Diamond Kafunguka


Ni siku saba zimepita sasa tangu Diamond Platnumz aiachie video yake mpya ambayo amewashirikisha P-Square.Video ambayo imefanikiwa kutazamwa na watu zaidi ya Milioni moja na laki tatu (1,300,000) hadi sasa ikiwa ilitimiza viewers zaidi ya milioni moja ndani ya muda wa siku nne tu.

Ndani ya video hiyo ameonekana mmoja kati ya wanyama wakali “SIMBA” jambo ambalo lilizua utata kwa waatazamaji kuweza kuamini ni jinsi gani Diamond alifanikiwa kushut na mnyama huyo huku ikieleweka kuwa balaa la mnyama huyo sio la kitoto.

Akiongea na Perfect 255 Diamond Platnumz na kupiga nae story kuhusu issue hiyo na haya hapa ndio majibu yake

“Aisee lile lilikuwa ni balaa, nasema ni balaa kwasababu kila mmoja baada ya kumuona mnyama yule ilibidi kwanza ake pembeni, na hadi kufikia hatua sisi kukaa nae vile ilibidi alishwe nyama nyingi sana ili asiweze kunitamani kabisa, muda si mrefu nitaweka behind the scene watu waweze kuona jinsi ilivyo kuwa,” Alisema
Diamond Platnumz

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni