.

Jumamosi, 23 Julai 2016

Kulihusu “BIFU” la chini chini kati ya Navy Kenzo na Weusi! Joh Makini ameyasema haya


Kumekuwa na tetesi zikiyahusisha makundi mawili ya muziki yanyo fanya vizuri sana kwasasa Navy Kenzo na Weusi kuwa makundi hayo yapo katika hali ya kutokuelewana (bifu).

Story hizo zimezuka baada ya wasanii wa kundi la weusi kuonekana kuwa wanafanya kazi katika studio tofauti na The Industry studio ambayo inamilikiwa na kundi la Navy Kenzo hali ambayo ni tofauti na awali makundi hayo yalionekana kushirikiana kwa kila kazi.

Joh Makini aliongea na Perfect255 nakuukanusha uvumi huo.

“Nilikuwa na Nahreel juzi na tumepiga story, sisi wenyewe tunashangaa kuzisikia hizi habari zimetoka wapi.

Mimi nilikuwa niki record studio nyingine hata kabla sijaanza kufanya kazi na Nahreel, na hata kama nilifanya kazi na Nahreel bado nilifanya kazi na maproducer wengine pia na watu walikuwa hawaongei.

Lakini siku zote watu huwa wanapenda habari za kubomoa kwasababu ndo zinakuwa zinahit, sijui kwanin mtu akifanya kitu kizuri huwa hakipewi nafasi.

Hali ambayo inaharibu hadi wasanii sasa, msanii yuko tayari kufanya kitu chochote ili apate nafasi ya kuzungumzwa.

Nafikiri watu waache kushabikia taarifa ambazo zinabomoa.

Alisema Joh Makini na kuwasisitiza wasanii waachane na habari za kiki na wajikite kwenye kuwekeza katika muziki mzuri.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni