.

Jumamosi, 23 Julai 2016

INDIA: WATU WAPEWA LIKIZO KWENDA KUSHUHUDIA UZINDUZI WA FILAMU


Wafanyakazi wengi kusini mwa India jana walipewa likizo kwa sababu ya filamu ya mwigizaji filamu inayoanza kuonyeshwa kwenye kumbi za sinema.

Filamu hiyo ni ya mwigizaji nyota wa asili ya Tamil, Rajinikanth.

Hatua hiyo imechukuliwa kuzuia watu kutumia visingizio kama vile kwamba wanaugua ili wasifike kazini.

Inahofiwa wengine huenda hata wangezima simu zao au kutofika kazini bila kueleza sababu.

Filamu hiyo kwa jina Kabali ilionyeshwa katika kumbi 12,000 za sinema jana.

Rajinikanth, ni mmoja wa waigizaji
wanaolipwa pesa nyingi sana bara Asia na mmoja wa waigizaji mashuhuri zaidi kutoka India.

Hata kabla ya kuzinduliwa, filamu hiyo ya Kabali, ambayo inaangazia uhalifu wa magenge, imejizolea $30m (Tsh 600m) kupitia mauzo ya haki zake.

Itatolewa pia kwa lugha za Kitelugu, Kihindi na Kimalay.

Katika miji kama vile Chennai na Bangalore, baadhi ya kampuni zilitangaza Ijumaa kuwa siku ya likizo na hata kuwapa wafanyakazi tiketi za bure wakatazame filamu hiyo.

Kampuni moja inasema ilichukua hatua hiyo kuzuia watu kufika kwa wingi wakiomba likizo siku ya jana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni