.

Alhamisi, 14 Julai 2016

Kituo cha polisi chavamiwa Kapenguria, Kenya


Maafisa kadha wa polisi wanahofiwa kufariki baada ya mtu mwenye silaha kushambulia kituo cha polisi eneo la Kapenguria, kaskazini magharibi mwa Kenya.

Mtu huyo anadaiwa kuvamia kituo hicho kumnusuru mshukiwa aliyekuwa amekamatwa akishukiwa kuhusika katika ugaidi, gazeti la Daily Nation limeripoti.
Gazeti hilo linasema huenda maafisa hadi watano wameuawa.

Mkuu wa polisi wa kituo hicho Vitalis Ochido anadaiwa kujeruhiwa.

Ufyatulianaji wa risasi bado unaendelea.
Tovuti ya habari ya Capital FM imemnukuu mkuu wa polisi Joseph Boinnet akisema polisi zaidi wametumwa eneo hilo.

“Mshukiwa wa ugaidi aliyekuwa anazuiliwa alitwaa bunduki na kuanza kuvyatua risasi," Bw Boinnet amenukuliwa. "Kituo hicho sasa kimezingirwa na juhudi za kukabiliana naye (mshambuliaji) zinaendelea.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni