.

Jumamosi, 16 Julai 2016

Hawa ndio wanahiphop wakubwa wanaopenda kucheza game ya Pokemon Go


Hivi karibuni kampuni ya Niantic Inc ilizindua game yake ya Pokemon Go ambayo imefanya kuwaweka raia wengi huko Marekani kuwa busy kuzunguka mitaani kucheza game hiyo, Miongoni mwa Rappers wenye majina makubwa duniani nao wamekuwa adicted kucheza game ya Pokemon Go.

Moja yaa vitu ambavyo vimefanya Game ya Pokemon Go kupendwa na kudownlodiwa na watu wengi, ni kwamba Game hiyo inatumia huduma ya GPS ambayo inamfanya mchezaji kuzunguka mtaani kupitia ramani ambayo inaonekana kwenye Game hiyo ili kuweza kujinyakulia baadhi ya vitu vinavyopatikana unapokuwa unatumia ramani ya Pokemon Go.

Pokemon Go imefanya baadhi ya wasanii wakubwa wa Hiphop kama Wiz Khalifa, Tyga, Waka Flocka Flame, Soulja Boy kujikuta wakiwa na mashabiki wao baada ya kucheza game hiyo wanapokuwa wanazunguka kwenye mitaa au miji kutafuta baadhi ya vikatuni ambavyo vinapatikana kwenye game hiyo.

Hizi ni post zilizopostiwa na Rappers wakubwa kuisifia game ya Pokemon Go.
Wiz Khalifa, Soulja Boy, Waka Flocka Flame, Tyga.

Kupitia mtandao wa Tmz ulimwonyesha Rapper Tyga akiwa upo busy anacheza Game ya Pokemon Go ambayo ilimfanya kutojali maongezi ya mpenzi wake Kylie Jenner.




Game ya Pokemon Go kwa sasa bado haijafika Bongo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni