.

Jumamosi, 16 Julai 2016

Diamond Platnumz: Nina miezi 12 ya kutusua nje ya Afrika


Usiku wa kuamkia jana yani usiku wa July 14 majira ya saa 3-4 usiku, msanii Diamond Platnumz alitoa muda wa lisaa lizima kwa mashabiki zake kuweza kuchat naye live na kumuuliza maswali yote ambayo wanajisikia kumuuliza nayeye kuwajibu papo hapo katika mtandao wa Instagram.

Hatua hiyo imekuja Baada ya video ya wimbo wake wa “Kidogo” kufanya vizuri ndani ya muda mfupi na kusifiwa kwa uwezo wake wa kurudisha furaha ya mashabiki wa kundi la P Square ambao walikuwa wakitamani wawaone wasanii hao wakiwa kwenye video pamoja.

Ni zaidi ya Comments 3800 zilipatikana ndani ya muda huo kutoka kwa mashabiki wa msanii huyo kumuuliza maswali mengi na wachache walifanikiwa kujibiwa maswali yao.

Moja kati ya maswali aliyo ulizwa Diamond Platnumz ni pamoja na

“Bro unafikiri muziki wako utachukua miaka mingapi ili ku hit marekani kama unavyo kick sasa Afrika!?” swali ambalo aliulizwa na shabiki wake anayetumia jina la @godfreymateru14 katika mtandao huo wa Instagram na Diamond Platnumz akamjibu”Inshaallah nipe miezi 12″

Swali lingine alilo ulizwa ni kwamba “Ni process gani ambazo msanii mchanga anatakiwa kuzitumia ili kuweza kafanya kazi na wasanii ambao anawasimamia yeye katika lebo yake ya WCB!? Wasanii kama Raymond, Harmonize na Rich Mavoko!”

“Awe mkali na awe na uwezo wa kushoot video bora na promo ya ngoma” Na hilo ndilo lilikuwa jibu la Diamond Platnumz kwa @romeoplatnumz_ ambaye ndiye alio muuliza swali hilo.



Ni kitu kizuri na kinafaa kuwa mfano wa kuigwa kwa wasanii wengine kuwa wanatoa muda wa kuzungumza na mashabiki zao kwasababu inasaidia kwa msanii kujua kilichomo katika fikra za mashabiki zake na kujua nini wana hitaji kwa wakati huo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni