.

Jumatatu, 18 Julai 2016

Fat joe kuwashirikisha tena French Montana na Remy Ma kwenye ngoma yake mpya


Fat Joe, Remy Ma na French Montana wanajipanga kuachia hit song nyingine ambayo itaitwa “Looks Like I’ve Been Cooking”, August 1 mwaka huu.

Ngoma ya “All the way up” ni ngoma ambayo imemfanya rapper Fat joe kufanya vizuri kwa mwaka huu tangu mara ya mwisho alipohit mwaka 2007, rapper Ramy Ma naye amejiandikia umaarufu mkubwa kupitia ngoma hiyo ambayo bado inajipatia umaarufu na kuingiza mkwanja mrefu.

Kupitia interview iliyofanywa na V-103 Atlanta, Fat joe alifunguka kuwa August mwaka huu anatarajia kuachia ngoma yake mpya ya “Looks Like I’ve Been Cooking” ambayo atawahusisha tena kwa mara nyingine French Montana na Remy Ma.

“New single August 1st. It’s called ‘Looks Like I’ve Been Cooking.’ If it ain’t broke don’t fix it. Me, Remy, and French We going out to Dubai to shoot the video next week. We’re gonna be acting real ignorant in the desert, and look for some white tigers.” alisema Fat joe.

Wimbo huo mashabiki watatarajia kuuona kwenye Album mpya za Fat joe na Remy Ma ambazo ni Plata o Plomo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni