.

Jumatatu, 20 Juni 2016

Yamoto Band wamedai kuwa walitengeneza kiki ya Aslay kutoka kimapenzi na Ruby ili wawashtue mashabiki wao


Kundi la muziki wa Bongo flava, Yamoto Band, wamefunguka na kusema kuwa iliwalazimu watengeneze kiki ya Aslay kutoka kimapenzi na Ruby ili kuwashtua mashabiki ambao walidai Yamoto band ilikuwa kimya kwa muda.

Wakizungumza kupitia kipindi cha The Playlist cha Times Fm, kiongozi wa Yamoto Aslay alidai kuwa walikuwa wakipokea lawama za mara kwa mara kuhusiana na ukimya wao kwenye Tasnia.

“Unajua kuna kipindi tulikuwa kimya mpaka watu walikuwa wakisema, so tukaamua tu tutengeneze ile ili kuvunja ukimya uliokuwa ukilalamikiwa” Alisema
Aslay.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni