.

Jumatano, 8 Juni 2016

Rita Ora amaliza mgogoro wake na Roc Nation ya Jay Z


Mwanamuziki wa Marekani, Rita Ora amemaliza mgogoro wake na label ya Roc Nation inayomilikiwa na Jay Z baada ya kupelekana mahakamani.

Rita Ora aliishitika Roc Nation mwishoni mwa mwaka jana kwa madai kutopromote kazi zake kwa kujihushisha zaidi na michezo, baadae label hiyo ilimfikisha kortini na yeye kwa madai kuwa hakukamilisha makubaliano ya mkataba wao, ilimtaka alipe dola milion 2.4

Mirror imeripoti kuwa mwanadada huyo amemaliza tofauti zake na label hiyo nje ya mahakama na sasa amesaini mkataba mpya na Warner Music.

Ora alisaini mkataba wa kurekodi album tano na Roc Nation mwaka 2008 . Hata hivyo amefanikiwa kutoa album moja tu, ORA ya mwaka 2012.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni