.

Jumatano, 8 Juni 2016

Abdu Kiba: Nipo tayari kufanya kazi na WCB, Mimi naangalia pesa tu


Tofauti za kimuziki za kaka yake Alikiba na Diamond hazina nafasi kwenye muziki wa Abdu Kiba ambaye amekiri yupo tayari kuingia kwenye label ya Diamond, WCB iwapo watakubaliana.

Akiongea na Planet Bongo ya EA Radio, Abdu Kiba amefunguka kuwa iwapo label hiyo [WCB] itakuwa na pesa za kutosha na makubaliano mazuri anaweza kufanya kazi chini yao.

“Nipo tayari naangalia pesa,” AbduKiba Alifunguka “Kama pesa zitakuwepo na wakihitaji kufanya kazi na mimi naweza nikafanya kazi chini ya lebo hiyo.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni